21 Na Yaeli mke wa Heberi akachukua kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake. Kisha akaenda kwake kimyakimya, akakipigilia kile kigingi katika kipaji cha uso wake,+ akakipigilia mpaka kikaingia katika udongo, huyo akiwa amelala usingizi mzito na kuchoka. Basi akafa.+