-
1 Wafalme 10:21, 22Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Vyombo vyote vya kunywea vya Mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya Nyumba ya Msitu wa Lebanoni+ vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu chochote kilichotengenezwa kwa fedha, kwa maana fedha ilionwa kuwa si kitu katika siku za Sulemani.+ 22 Mfalme alikuwa na kundi la meli za Tarshishi+ baharini pamoja na kundi la meli za Hiramu. Mara moja baada ya kila miaka mitatu, kundi la meli za Tarshishi zilikuja zikiwa zimejazwa dhahabu na fedha, pembe za tembo,+ sokwe, na tausi.
-