Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 7/8 kur. 3-4
  • Ubashiri-Nyota Leo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ubashiri-Nyota Leo
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Uvutio Huo?
  • Je, Unajimu Unaweza Kukufunulia Wakati Ujao?
    Amkeni!—2005
  • Je! Kweli Nyota Hudhibiti Maisha Yako?
    Amkeni!—1990
  • Nyota Zina Habari Gani Kwako?
    Amkeni!—1994
  • Je, Maisha Yako Yanaongozwa na Nyota?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 7/8 kur. 3-4

Ubashiri-Nyota Leo

“KUTOKA [ikulu ya] White House hadi Wall Street, unajimu haujapata kamwe kuwa maarufu kama ulivyo sasa.” Ndivyo ilivyoanza ripoti moja ya gazeti juu ya upendezi wa umma katika unajimu katika United States.

Bila shaka kutajwa kwa White House kulikumbusha msomaji usimulizi ule uliotangazwa sana na mmoja aliyekuwa mtekelezi wa mashauri ya rais. Katika kitabu chake For the Record, Donald T. Regan aliandika hivi:

“Karibu kila hatua au uamuzi mkubwa uliofanywa na akina Reagan wakati nilipokuwa mkuu wa wafanya kazi wa White House ulichunguzwa mapema pamoja na mwanamke mmoja katika San Francisco aliyepiga falaki kuhakikisha kwamba sayari zilipatana na shughuli ile.”

Hata kama kuna maoni mengineyo yawezayo kukatwa kutokana na usimulizi huo, hakika yalishiriki sana kujulisha wazi upendezi mkubwa sana wa unajimu ulio miongoni mwa watu katika ulimwengu wa Magharibi, ambako sayansi ya ki-siku-hizi yasemwa kuwa iliondolea mbali unajimu wa mwisho uliokuwa umebakia. Fikiria mambo ya hakika:

◼ Kulingana na AFA (Shirika la Wanajimu Amerika), katika United States kuna wanajimu karibu 5,000 wenye kazi ya wakati wote na angalau 50,000 wenye kazi ya nusu-wakati. Kwa mwaka, malipo ya kusomewa ubashiri hujumlika kuwa karibu dola milioni 35.

◼ “Kila mwaka katika Ufaransa . . . watu zaidi ya milioni 10 hutafuta ushauri kwa mmoja wa wale wanajimu au wawasilisha-habari zaidi ya 30,000 wanaotambuliwa kirasmi,” lasema Toutes les Nouvelles, gazeti la kila juma la Paris.

◼ Falaki ni sehemu ya kawaida katika asilimia 92, au magazeti zaidi ya 1,500, ya magazeti ya kila siku katika United States. Katika Ujeremani, ambako gazeti moja la kila siku, Weser Kurier, halikuchapa safu ya falaki siku moja, simu zilipokewa kutoka kwa wasomaji “ambao hawakujua kama watakaa nyumbani au wataenda nje mchana huo, kama wataweka pesa zao katika rasilmali, na ikiwa ndivyo waziweke wapi.”

◼ Wanajimu wengi zaidi na zaidi wanageukia kompyuta. Kwa kielelezo, shirika Astro Intelligence la Uswisi laweza kuandaa uchanganuzi wa kurasa 20 zenye kuchapwa na kompyuta kwa gharama ya faranga 55 za Kiswisi (dola 36 za United States). Mnajimu mmoja Mwingereza ajulikanaye sana hupeleka nje falaki ya kibinafsi zaidi ya 20,000 kwa mwaka kwa karibu pauni 10 (dola 18 za United States) kila mmoja. Hata huduma za kueleza falaki katika simu zinaanza kupatikana sasa katika majiji kama New York. Kampuni ya Simu New York yaripoti kwamba simu karibu milioni moja hupokewa kila mwezi.

Kwa Nini Uvutio Huo?

Katika muda huu wa kujitoshelezea tamaa za kibinafsi, kitu chochote chenye kuahidi uandalizi wa muono-ndani mzuri zaidi katika maana ya maisha au uelewevu mzuri zaidi juu ya mtu binafsi kitakubaliwa tu. Hivyo, kulingana na maneno ya mtazamaji mmoja, moja ya sababu ambazo watu huvutiwa na unajimu ni kwamba “huo hudai kukueleza wewe juu ya mtu aliye wa maana kupita wote, wewe mwenyewe.”

Lakini je! kweli unajimu hufanya hivyo? Na, kwa umaana mkubwa zaidi, kweli nyota hudhibiti maisha zetu? Acheni tuitazame ajabu hii kwa ukaribu zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki