Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w10 4/1 uku. 4
  • Yesu Kristo—Nguvu ya Ujumbe Wake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Kristo—Nguvu ya Ujumbe Wake
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Iweni Watendaji wa Neno, Si Wasikiaji Tu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Acha Maneno ya Yesu Yafinyange Mtazamo Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • “Mtu Mwingine Hajapata Kamwe Kusema Kama Huyu”
    ‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
  • Miujiza Ambayo Yesu Alifanya Katika Mji Alimokaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
w10 4/1 uku. 4

Yesu Kristo—Nguvu ya Ujumbe Wake

“Bila shaka jambo linalothibitisha kwamba mtu huyu mwenye hekima kutoka Kapernaumu alikuwa mtu wa pekee ni kwamba bado watu wanauamini na kuupenda ujumbe wake.”a—MWANDISHI GREGG EASTERBROOK.

MANENO yana nguvu. Yanapochaguliwa vizuri, yanaweza kuchochea mioyo ya watu, kuwapa tumaini, na kubadili maisha yao. Hakuna mtu mwingine ambaye amewahi kusema maneno yenye nguvu kama Yesu Kristo. Mtu fulani aliyesikiliza Mahubiri ya Mlimani ya Yesu, aliandika hivi baadaye: “Basi wakati Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati ukashangazwa na njia yake ya kufundisha.”—Mathayo 7:28.

Mpaka leo hii, watu duniani kote wanajua semi nyingi za Yesu. Fikiria baadhi ya semi zake zenye kujaa maana.

“Hamwezi kutumikia Mungu na Utajiri.”—Mathayo 6:24.

“Mambo yote mnayotaka watu wawatendee ninyi, lazima mwatendee wao pia vivyo hivyo.”—Mathayo 7:12.

“Mlipeni Kaisari vitu vya Kaisari, lakini Mungu vitu vya Mungu.”—Mathayo 22:21.

“Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.”—Matendo 20:35.

Yesu alifanya mengi zaidi ya kusema semi muhimu na zisizosahaulika. Ujumbe aliohubiri ulikuwa wenye nguvu kwa sababu ulifunua ukweli kumhusu Mungu, uliwapa watu kusudi maishani, na ulionyesha wazi kwamba suluhisho la matatizo ya wanadamu ni Ufalme wa Mungu. Tunapochunguza mafundisho ya Yesu katika kurasa zinazofuata, tutaona kwa nini mamilioni ya watu bado “wanauamini na kuupenda ujumbe wake.”

[Maelezo ya Chini]

a Kapernaumu lilionwa kuwa jiji la nyumbani la Yesu katika eneo la Galilaya.—Marko 2:1.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki