Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Simulizi la Mito Miwili
    Amkeni!—2000 | Julai 8
    • Simulizi la Mito Miwili

      NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA INDIA

      Mito miwili iliyo muhimu kwa uhai katika bara Hindi, huandaa riziki kwa mamia ya mamilioni ya watu. Kila mto huanzia kwenye maeneo ya barafu ya safu ya milima mirefu zaidi ulimwenguni, na kutiririka taratibu kwa umbali wa zaidi ya kilometa 2,400 kupitia nchi mbili. Mito hiyo huishia katika bahari mbili tofauti. Kila mto ulikuwa chimbuko la ustaarabu wa kale. Kila mto ulihusiana na kuanza kwa dini kuu. Kila mto huthaminiwa na wanadamu kwa sababu ya faida zake, na mmoja unaabudiwa, hata leo. Inaitwaje? Mto Indus na Ganges, huo wa mwisho huitwa Ganga hapa India.

      USTAARABU wa kale ulianzia karibu na mito kwa sababu maji ni muhimu kwa uhai na usitawi wa mwanadamu. Mambo hakika ya kale yaweza kufichwa na hekaya kwa sababu nyakati nyingine mito ilionwa kuwa miungu ya kiume na miungu ya kike. Ndivyo ilivyo kuhusu historia ya Mto Indus na Ganga, ambao pia huitwa Ganga Ma (Mama Ganga) hapa India.

      Mlima Kailash wenye urefu wa meta 6,714 na Ziwa Manasarovar lililo karibu, huonwa na Wahindi na Wabudha kuwa makao ya miungu. Kwa muda mrefu, iliaminika kuwa mito mikubwa minne ilitiririka kutoka kwenye vinywa vya wanyama ziwani. Indus ulikuwa mto wa simba, na Ganga ulikuwa mto wa tausi.

      Watibet hawakuwakaribisha wavumbuzi wageni. Hata hivyo, mnamo mwaka wa 1811, daktari Mwingereza aliye mpasuaji wa mifugo ambaye aliajiriwa na East India Company alivinjari nchini kwa kujificha. Aliripoti kwamba hakuna mito yoyote iliyotiririka kutoka kwa Manasarovar, ingawa vijito kadhaa kutoka milimani viliingia ndani yake. Vyanzo vya Mto Indus na Ganga vilivumbuliwa mwanzoni mwa karne ya 20 tu. Mto Indus huanzia Tibet, kaskazini ya Milima ya Himalaya, na Ganga huanzia kwenye pango la barafu katika miteremko ya milima ya Himalaya kaskazini mwa India.

  • Simulizi la Mito Miwili
    Amkeni!—2000 | Julai 8
    • Boma la Farakka, kwenye Mto Ganga, huhifadhi maji ya kutosha kwa ajili ya kuongezeka kwa usafiri wa meli karibu na Bandari ya Calcutta.

      Sawa na mito mingine, uchafuzi ni tatizo kubwa kwenye Mto Ganga. Hivyo, mnamo 1984 Mpango madhubuti wa Kuhifadhi Mto Ganga ulianzishwa na serikali ya India. Ulikazia kufanyiza mbolea au biogesi kutokana na maji machafu, kuzuia maji machafu yanayoingia mtoni, na kutengeneza viwanda vya kuondoa uchafu wa kemikali.

  • Simulizi la Mito Miwili
    Amkeni!—2000 | Julai 8
    • Makabila fulani ya Kiarya yalielekea mashariki mwa India na kuishi katika uwanda wa Mto Ganga. Hivyo wakazi Waarya wa barani walianzisha utamaduni wao wa pekee kaskazini mwa India, ulioshirikishwa hasa na Mto Ganga, na ungalipo leo.

  • Simulizi la Mito Miwili
    Amkeni!—2000 | Julai 8
    • Huku Uhindu ukianzia karibu na Mto Indus, Ubudha ulianzia karibu na Mto Ganga. Siddhārtha Gautama aitwaye Buddha, alianza mahubiri yake ya kwanza katika Sarnath, karibu na Varanasi. Yasemekana kwamba aliogelea na kuvuka sehemu pana ya Mto Ganga alipokuwa na umri wa miaka 79.

      Mito Hiyo Ikoje Leo?

      Maji ya mto ni muhimu sana leo kuliko yalivyokuwa miaka 4,000 iliyopita, watu walipohamia kwenye kingo za Mto Indus na Ganga ili kujiruzuku. Ni sharti mito hiyo isimamiwe kwa uangalifu ili iweze kuruzuku wakazi wengi wa India, Pakistan, na Bangladesh. (Ona ramani kwenye ukurasa wa 16-17.) Mikataba ya kimataifa imehitaji kufanywa kwa kuwa mito hiyo hupita katika nchi kadhaa.

  • Simulizi la Mito Miwili
    Amkeni!—2000 | Julai 8
    • Mto Ganga Unaoheshimiwa Sana

      Mto Ganga wenye urefu wa zaidi ya kilometa 2,500 huanzia upande wa kusini wa chanzo cha Mto Indus umbali wa kilometa 100 hivi kwenye milima ya Himalaya, nao hutiririka hadi kwenye Ghuba ya Bengal. Kwenye mwinuko wa zaidi ya meta 3,870, chemchemi ya kijito kinachoitwa Bhagirathi hububujika kutoka kwenye kilima cha barafu kinachoshabihi kinywa cha ng’ombe, ambacho huitwa kwa Kihindi Gaumukh. Huungana na kijito kingine kiitwacho Alaknanda, huko Devaprayag zapata kilometa 214 hivi kutoka kwenye chanzo chake. Vijito hivyo viwili pamoja na Mandakini, Dhauliganga, na Pindar hufanyiza Mto Ganga.

      Mto Ganga uelekeapo kusini-mashariki na kuvuka bara hilo, huungana na mito mingine mikubwa kama vile Yamuna katika Allahabad huko India kisha Brahmaputra wenye nguvu huko Bangladesh. Huku ukiwa umesambaa kama feni, Mto Ganga na mito midogo inayoingia ndani yake hueneza maji kwenye robo ya eneo lote la India, katika uwanda wenye rutuba wa Ganga. Mfumo huo wa mito hukusanya maji kutoka kwenye eneo la kilometa 1,035,000 za mraba na hutegemeza theluthi ya watu wote India, ambao idadi hiyo sasa inapita bilioni moja, katika mojawapo ya maeneo yaliyosongamana zaidi ulimwenguni. Hupanuka sana ufikapo Bangladesh, mfano wa bahari iliyo barani, huwa na vyombo vya usafiri wa majini vya kila namna. Kisha Mto Ganga hugawanyika na kutokeza mito kadhaa muhimu na vijito vingi na kuwa mojawapo ya delta kubwa zaidi ulimwenguni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki