-
Mwanzo 16:1, 2Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
16 Sasa Sarai mke wa Abramu hakuwa amemzalia mtoto yeyote,+ lakini alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Hagari.+ 2 Basi Sarai akamwambia Abramu: “Sasa tafadhali! Yehova amenizuia nisizae watoto. Tafadhali, lala na mtumishi wangu. Huenda nikapata watoto kupitia yeye.”+ Kwa hiyo Abramu akasikiliza maneno ya Sarai.
-
-
Mwanzo 30:9Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
9 Lea alipoona kwamba ameacha kuzaa, alimchukua Zilpa kijakazi wake na kumpa Yakobo awe mke wake.+
-
-
Mwanzo 46:18Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
18 Hao ndio wana wa Zilpa,+ kijakazi ambaye Labani alimpa Lea binti yake. Alimzalia Yakobo wana hao: wote walikuwa 16.
-