-
Mambo ya Walawi 4:11, 12Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
11 “‘Lakini ngozi ya ng’ombe dume huyo na nyama yake yote pamoja na kichwa chake, miguu yake, matumbo yake, na mavi yake+— 12 sehemu zote zinazobaki za ng’ombe dume huyo—atazipeleka mahali safi nje ya kambi, mahali ambapo majivu* hutupwa, naye ataziteketeza kwa moto juu ya kuni.+ Zinapaswa kuteketezwa mahali ambapo majivu hutupwa.
-
-
Mambo ya Walawi 16:27Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
27 “Yule ng’ombe dume wa dhabihu ya dhambi na yule mbuzi wa dhabihu ya dhambi, ambao damu yao ililetwa mahali patakatifu ili itumiwe kufunika dhambi, watapelekwa nje ya kambi, na ngozi zao na nyama yao na mavi yao vitateketezwa motoni.+
-