-
Kumbukumbu la Torati 4:9Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
9 “Ila tu muwe waangalifu na kujihadhari sana, ili msisahau mambo ambayo macho yenu yameona na ili yasiondoke moyoni mwenu siku zote za maisha yenu. Ni lazima pia muwaambie wana wenu na wajukuu wenu.+
-
-
Kumbukumbu la Torati 6:21Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
21 ndipo utakapomwambia mwana wako, ‘Tulikuwa watumwa wa Farao kule Misri, lakini Yehova alitutoa Misri kwa mkono wenye nguvu.
-
-
Kumbukumbu la Torati 11:18, 19Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
18 “Ni lazima uyakazie maneno haya yangu katika moyo wako na nafsi* yako na kuyafunga kama kumbukumbu kwenye mkono wako, nayo yanapaswa kuwa kama utepe kwenye paji la uso wako.*+ 19 Wafundishe watoto wako maneno haya, na kuongea kuyahusu unapoketi nyumbani mwako na unapotembea barabarani na unapolala na unapoamka.+
-