-
Kutoka 7:20Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
20 Mara moja Musa na Haruni wakafanya kama Yehova alivyowaamuru. Akaiinua fimbo hiyo na kuyapiga maji ya Mto Nile mbele ya Farao na watumishi wake, na maji yote yaliyokuwa katika Mto Nile yakabadilika na kuwa damu.+
-
-
Kutoka 8:6Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
6 Basi Haruni akaunyoosha mkono wake juu ya maji ya Misri, na vyura wakaanza kuja na kuifunika nchi ya Misri.
-
-
Kutoka 8:17Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
17 Nao wakafanya hivyo. Haruni akaunyoosha mkono wake uliokuwa na fimbo yake na kuyapiga mavumbi ya ardhi, na mbu wakawavamia wanadamu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi yote ya Misri yakawa mbu.+
-
-
Kutoka 9:6Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
6 Na kesho yake Yehova akafanya hivyo, kila aina ya mifugo ya Wamisri ikaanza kufa,+ lakini hakuna mnyama hata mmoja wa Waisraeli aliyekufa.
-
-
Kutoka 9:10Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
10 Basi wakachukua masizi kutoka katika tanuru* na kusimama mbele ya Farao, naye Musa akayarusha hewani, nayo yakawa majipu yenye usaha yaliyotokea kwenye miili ya wanadamu na wanyama.
-
-
Kutoka 9:23Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
23 Kwa hiyo Musa akainyoosha fimbo yake kuelekea mbinguni, na Yehova akaleta ngurumo na mvua ya mawe, na moto* ukashuka duniani, na Yehova akafanya mvua ya mawe iendelee kunyesha juu ya nchi ya Misri.
-
-
Kutoka 10:12Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
12 Sasa Yehova akamwambia Musa: “Unyooshe mkono wako juu ya nchi ya Misri ili nzige waje juu ya nchi ya Misri na kula mimea yote nchini, kila kitu ambacho hakikuharibiwa na mvua ya mawe.”
-
-
Kutoka 10:21Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
21 Basi Yehova akamwambia Musa: “Unyooshe mkono wako kuelekea mbinguni ili giza liifunike nchi ya Misri, giza zito sana hivi kwamba linaweza kuguswa.”
-