-
Yeremia 41:16Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
16 Yohanani mwana wa Karea na wakuu wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawachukua watu waliobaki Mispa ambao walikuwa wamewaokoa kutoka kwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada ya kumuua Gedalia+ mwana wa Ahikamu. Wakawaleta wanaume, wanajeshi, wanawake, watoto, na maofisa wa makao ya mfalme kutoka Gibeoni.
-
-
Yeremia 42:1-3Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
42 Kisha wakuu wote wa jeshi, na Yohanani+ mwana wa Karea, Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote, kuanzia mdogo zaidi mpaka mkubwa zaidi, wakakaribia 2 na kumwambia nabii Yeremia: “Tafadhali, sikia ombi letu la kutaka kibali nawe usali kwa ajili yetu kwa Yehova Mungu wako, kwa ajili ya watu hawa wote waliobaki, kwa maana kati ya watu wengi, wachache ndio waliobaki,+ kama unavyoona. 3 Yehova Mungu wako na atuambie njia tunayopaswa kuifuata na jambo tunalopaswa kufanya.”
-