-
2 Wafalme 23:8, 9Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
8 Kisha akawaondoa makuhani wote katika majiji ya Yuda, naye akafanya mahali pa juu ambapo makuhani walifukizia moshi wa dhabihu pasifae kwa ibada, kuanzia Geba+ mpaka Beer-sheba.+ Alibomoa pia mahali pa juu palipokuwa kwenye malango yaliyokuwa katika njia ya kuingia kwenye lango la Yoshua mkuu wa jiji, malango yaliyokuwa upande wa kushoto mtu anapoingia katika lango la jiji. 9 Makuhani wa mahali pa juu hawakuhudumu kwenye madhabahu ya Yehova kule Yerusalemu,+ lakini walikula mikate isiyo na chachu pamoja na ndugu zao.
-
-
Nehemia 9:34Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
34 Wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, na mababu zetu hawajashika Sheria yako wala kusikiliza amri zako wala vikumbusho ulivyowapa* ili kuwaonya.
-
-
Ezekieli 8:5Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
5 Kisha akaniambia: “Mwana wa binadamu, tafadhali inua macho yako kuelekea kaskazini.” Basi nikainua macho yangu kuelekea kaskazini, na huko, upande wa kaskazini wa lango la madhabahu kulikuwa na ishara hii ya* wivu langoni.
-