Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 3
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ayubu—Yaliyomo

      • Ayubu ajuta kuzaliwa (1-26)

        • Auliza kwa nini anateseka (20, 21)

Ayubu 3:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kuilaani siku yake.”

Marejeo

  • +Yer 20:14, 15

Ayubu 3:3

Marejeo

  • +Ayu 10:18, 19; Yer 15:10

Ayubu 3:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “giza na kivuli cha kifo.”

Ayubu 3:6

Marejeo

  • +Ayu 10:18, 19

Ayubu 3:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Inaeleweka kwamba maneno haya yanamrejelea mamba au mnyama mwingine mkubwa mwenye nguvu anayekaa ndani ya maji.

Marejeo

  • +Ayu 41:1, 10; Zb 104:25, 26

Ayubu 3:10

Marejeo

  • +Ayu 10:18

Ayubu 3:11

Marejeo

  • +Yer 20:17, 18

Ayubu 3:13

Marejeo

  • +Mhu 9:5, 10
  • +Yoh 11:11

Ayubu 3:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “Waliojijengea mahali palipo ukiwa.”

Ayubu 3:17

Marejeo

  • +Zb 146:4; Mhu 9:10; Isa 57:1, 2

Ayubu 3:19

Marejeo

  • +Ayu 30:23; Zb 49:10, 12; Mhu 8:8; 9:2

Ayubu 3:20

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “wale walio na uchungu nafsini.”

Marejeo

  • +1Sa 1:10; 2Fa 4:27

Ayubu 3:21

Marejeo

  • +Hes 11:11, 15; 1Fa 19:3, 4; Ayu 7:15, 16; Yon 4:2, 3

Ayubu 3:23

Marejeo

  • +Ayu 12:14; 19:8

Ayubu 3:24

Marejeo

  • +Zb 102:9, 10
  • +Zb 22:1; 38:8

Jumla

Ayu. 3:1Yer 20:14, 15
Ayu. 3:3Ayu 10:18, 19; Yer 15:10
Ayu. 3:6Ayu 10:18, 19
Ayu. 3:8Ayu 41:1, 10; Zb 104:25, 26
Ayu. 3:10Ayu 10:18
Ayu. 3:11Yer 20:17, 18
Ayu. 3:13Mhu 9:5, 10
Ayu. 3:13Yoh 11:11
Ayu. 3:17Zb 146:4; Mhu 9:10; Isa 57:1, 2
Ayu. 3:19Ayu 30:23; Zb 49:10, 12; Mhu 8:8; 9:2
Ayu. 3:201Sa 1:10; 2Fa 4:27
Ayu. 3:21Hes 11:11, 15; 1Fa 19:3, 4; Ayu 7:15, 16; Yon 4:2, 3
Ayu. 3:23Ayu 12:14; 19:8
Ayu. 3:24Zb 102:9, 10
Ayu. 3:24Zb 22:1; 38:8
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ayubu 3:1-26

Ayubu

3 Baada ya hayo Ayubu alianza kuongea na kuilaani siku aliyozaliwa.*+ 2 Ayubu akasema:

 3 “Na itokomee siku niliyozaliwa,+

Pia usiku ambao mtu alisema: ‘Mimba iliyotungwa ni ya mwanamume!’

 4 Siku hiyo na iwe giza.

Mungu aliye juu asiihangaikie siku hiyo;

Na nuru isiiangazie.

 5 Na imilikiwe na giza zito sana.*

Wingu la mvua na litande juu yake.

Na chochote kinacholeta giza mchana kiitie hofu siku hiyo.

 6 Usiku huo—na ushikwe na giza;+

Na isishangilie miongoni mwa siku nyingine za mwaka,

Nayo isihesabiwe miongoni mwa siku za miezi.

 7 Kwa kweli! Usiku huo na uwe tasa;

Kelele za shangwe zisisikiwe usiku huo.

 8 Wale wanaolaani siku na wailaani,

Wale wanaoweza kumwamsha Lewiathani.*+

 9 Nyota zake za alfajiri na ziwe giza;

Usiku huo ungojee nuru bila mafanikio,

Nao usione miale ya mapambazuko.

10 Kwa maana haukufunga milango ya tumbo la uzazi la mama yangu;+

Wala haukuficha taabu kutoka machoni pangu.

11 Kwa nini sikufa nilipozaliwa?

Kwa nini sikuangamia nilipotoka tumboni?+

12 Kwa nini mama yangu alinipakata mapajani

Na kuninyonyesha?

13 Kwa maana sasa ningekuwa nimelala chini bila usumbufu;+

Ningekuwa nimelala na kupumzika+

14 Pamoja na wafalme wa dunia na washauri wao,

Waliojijengea majengo ambayo sasa ni magofu,*

15 Au pamoja na wakuu waliomiliki dhahabu,

Ambao nyumba zao zilijaa fedha.

16 Au kwa nini sikuwa kama mimba iliyoharibika ambayo imefichika,

Kama watoto ambao hawajawahi kamwe kuona nuru?

17 Katika kifo hata waovu hawasumbui tena;

Na humo waliochoka hupumzika.+

18 Humo wafungwa hukaa pamoja kwa utulivu;

Hawasikii sauti ya mtu anayewalazimisha kufanya kazi.

19 Humo wadogo ni sawa na wakubwa,+

Na humo mtumwa yuko huru kutoka kwa bwana wake.

20 Kwa nini anampa nuru anayeteseka

Na kuwapa uhai wale wanaoteseka kwa uchungu mwingi?*+

21 Kwa nini wanatamani sana kifo, lakini hakiji?+

Wanachimba wakikitafuta kuliko hazina zilizofichika,

22 Wale wanaoshangilia sana,

Wanaofurahi wanapopata kaburi.

23 Kwa nini anampa nuru mwanamume aliyepotea njia,

Ambaye Mungu amemzingira kwa ukuta?+

24 Kwa maana badala ya chakula changu majonzi hunijia,+

Na kilio changu cha uchungu+ humwagika kama maji.

25 Kwa maana ninachoogopa sana kimenijia,

Na ninachohofu kimenipata.

26 Sijawa na amani, wala utulivu, wala sijapumzika,

Lakini taabu inaendelea kuniandama.”

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki