Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yoshua 20
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Yoshua—Yaliyomo

      • Majiji ya makimbilio (1-9)

Yoshua 20:2

Marejeo

  • +Kut 21:12, 13; Hes 35:14, 15; Kum 4:41

Yoshua 20:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “anayeua nafsi.”

Marejeo

  • +Mwa 9:6; Kut 21:23; Hes 35:26, 27

Yoshua 20:4

Marejeo

  • +Kum 19:3
  • +Met 31:23

Yoshua 20:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “bila kujua.”

Marejeo

  • +Hes 35:22-24; Kum 19:4-6

Yoshua 20:6

Marejeo

  • +Hes 35:12, 24
  • +Hes 35:25
  • +Hes 35:28

Yoshua 20:7

Marejeo

  • +Yos 21:32
  • +Mwa 33:18; Yos 21:20, 21
  • +Yos 14:15; 21:13

Yoshua 20:8

Marejeo

  • +Yos 21:8, 36; 1Nya 6:77, 78
  • +Yos 21:8, 38; 1Nya 6:77, 80
  • +Yos 21:27; 1Nya 6:71
  • +Kum 4:41-43

Yoshua 20:9

Marejeo

  • +Hes 35:11, 15
  • +Hes 35:12, 24; Kum 21:5

Jumla

Yos. 20:2Kut 21:12, 13; Hes 35:14, 15; Kum 4:41
Yos. 20:3Mwa 9:6; Kut 21:23; Hes 35:26, 27
Yos. 20:4Kum 19:3
Yos. 20:4Met 31:23
Yos. 20:5Hes 35:22-24; Kum 19:4-6
Yos. 20:6Hes 35:12, 24
Yos. 20:6Hes 35:25
Yos. 20:6Hes 35:28
Yos. 20:7Yos 21:32
Yos. 20:7Mwa 33:18; Yos 21:20, 21
Yos. 20:7Yos 14:15; 21:13
Yos. 20:8Yos 21:8, 36; 1Nya 6:77, 78
Yos. 20:8Yos 21:8, 38; 1Nya 6:77, 80
Yos. 20:8Yos 21:27; 1Nya 6:71
Yos. 20:8Kum 4:41-43
Yos. 20:9Hes 35:11, 15
Yos. 20:9Hes 35:12, 24; Kum 21:5
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Yoshua 20:1-9

Yoshua

20 Kisha Yehova akamwambia Yoshua: 2 “Waambie Waisraeli, ‘Jichagulieni majiji ya makimbilio+ kama nilivyowaambia kupitia Musa, 3 ili mtu atakayemuua mwenzake* bila kukusudia au bila kujua akimbilie humo. Atakimbilia humo ili kumkwepa mtu anayetaka kulipiza kisasi cha damu.+ 4 Ni lazima akimbilie mojawapo ya majiji hayo+ na kusimama langoni,+ kisha atawaambia wazee wa jiji hilo kesi yake. Nao lazima wampokee jijini na kumpa makao, naye ataishi pamoja nao. 5 Na yule anayetaka kulipiza kisasi cha damu akimfuatia, wazee hawapaswi kumtia muuaji huyo mikononi mwake, kwa maana alimuua mwenzake bila kukusudia,* wala hakuwa akimchukia.+ 6 Ni lazima akae ndani ya jiji hilo mpaka kesi yake itakaposikilizwa mbele ya kusanyiko,+ naye atabaki humo mpaka kuhani mkuu+ anayehudumu wakati huo atakapokufa. Kisha muuaji huyo anaweza kurudi nyumbani kwake katika jiji alilokimbia.’”+

7 Basi wakatenga majiji haya kuwa matakatifu: Kedeshi+ kule Galilaya katika eneo lenye milima la Naftali, Shekemu+ katika eneo lenye milima la Efraimu, na Kiriath-arba,+ yaani, Hebroni, katika eneo lenye milima la Yuda. 8 Na katika eneo la Yordani, upande wa mashariki wa Yeriko, wakachagua jiji la Beseri+ lililo nyikani kwenye uwanda wa juu katika eneo la kabila la Rubeni, Ramothi+ kule Gileadi katika eneo la kabila la Gadi, na Golani+ kule Bashani katika eneo la kabila la Manase.+

9 Hayo ndiyo majiji yaliyochaguliwa kwa ajili ya Waisraeli wote na wageni walioishi kati yao, ili mtu yeyote atakayemuua mwenzake bila kukusudia akimbilie humo,+ ili asiuawe na mtu anayetaka kulipiza kisasi cha damu mpaka kesi yake isikilizwe mbele ya kusanyiko.+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki