Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 5
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Sanduku la agano katika eneo la Wafilisti (1-12)

        • Dagoni aaibishwa (1-5)

        • Wafilisti waletewa pigo (6-12)

1 Samweli 5:1

Marejeo

  • +1Sa 4:11

1 Samweli 5:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “hekalu la.”

Marejeo

  • +Amu 16:23; 1Nya 10:8-10

1 Samweli 5:3

Marejeo

  • +Kut 12:12; 1Nya 16:26; Zb 97:7
  • +Isa 46:6, 7

1 Samweli 5:4

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Ni Dagoni tu aliyebaki.”

1 Samweli 5:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “ulikuwa mzito dhidi ya.”

  • *

    Au “ugonjwa wa puru.”

Marejeo

  • +1Sa 6:5, 6

1 Samweli 5:8

Marejeo

  • +1Sa 17:4

1 Samweli 5:9

Marejeo

  • +1Sa 5:6

1 Samweli 5:10

Marejeo

  • +Yos 15:20, 45; 2Fa 1:2; Amo 1:8
  • +1Sa 5:7

1 Samweli 5:11

Marejeo

  • +1Sa 5:6, 9

Jumla

1 Sam. 5:11Sa 4:11
1 Sam. 5:2Amu 16:23; 1Nya 10:8-10
1 Sam. 5:3Kut 12:12; 1Nya 16:26; Zb 97:7
1 Sam. 5:3Isa 46:6, 7
1 Sam. 5:61Sa 6:5, 6
1 Sam. 5:81Sa 17:4
1 Sam. 5:91Sa 5:6
1 Sam. 5:10Yos 15:20, 45; 2Fa 1:2; Amo 1:8
1 Sam. 5:101Sa 5:7
1 Sam. 5:111Sa 5:6, 9
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
1 Samweli 5:1-12

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

5 Wafilisti walipoliteka Sanduku la Mungu+ wa kweli walilibeba kutoka Ebenezeri mpaka Ashdodi. 2 Wafilisti wakalichukua Sanduku la Mungu wa kweli, wakaliingiza ndani ya nyumba ya* Dagoni na kuliweka kando ya Dagoni.+ 3 Siku iliyofuata Waashdodi walipoamka asubuhi na mapema, walimkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Yehova.+ Basi wakamchukua Dagoni na kumrudisha mahali pake.+ 4 Walipoamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, walimkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Yehova. Kichwa cha Dagoni na vitanga vya mikono yake miwili vilikuwa vimekatwa, navyo vilikuwa chini kwenye kizingiti. Ni sehemu tu yenye umbo la samaki ndiyo iliyobaki.* 5 Ndiyo sababu mpaka leo hii, makuhani wa Dagoni na wote wanaoingia katika nyumba ya Dagoni hawakanyagi kizingiti cha Dagoni kule Ashdodi.

6 Mkono wa Yehova uliwaadhibu vikali* Waashdodi, naye akawaangamiza kwa kuleta bawasiri* huko Ashdodi na katika maeneo yake.+ 7 Watu wa Ashdodi walipoona mambo yaliyokuwa yakitukia wakasema: “Msiruhusu Sanduku la Mungu wa Israeli likae pamoja nasi, kwa sababu mkono wake umetuadhibu vikali sisi pamoja na mungu wetu Dagoni.” 8 Basi wakatuma ujumbe na kuwakusanya watawala wote wa Wafilisti na kuwauliza: “Tulifanyie nini Sanduku la Mungu wa Israeli?” Wakajibu: “Acheni Sanduku la Mungu wa Israeli lihamishiwe kule Gathi.”+ Basi wakalihamishia huko Sanduku la Mungu wa Israeli.

9 Baada ya kulihamishia huko, mkono wa Yehova ukaja dhidi ya jiji hilo, na kusababisha hofu kubwa. Akawapiga wanaume wa jiji hilo, kuanzia mdogo mpaka mkubwa, wakatokwa na majipu ya bawasiri.+ 10 Basi wakalipeleka Sanduku la Mungu wa kweli kule Ekroni,+ lakini mara tu Sanduku la Mungu wa kweli lilipofika Ekroni, Waekroni wakaanza kulia kwa sauti wakisema: “Wametuletea Sanduku la Mungu wa Israeli ili watuue sisi pamoja na watu wetu!”+ 11 Kwa hiyo wakatuma ujumbe na kuwakusanya watawala wote wa Wafilisti na kuwaambia: “Liondoeni hapa Sanduku la Mungu wa Israeli; lirudisheni mahali pake ili sisi pamoja na watu wetu tusiuawe.” Kwa maana hofu ya kifo ilikuwa imeenea katika jiji lote; mkono wa Mungu wa kweli ulikuwa umewaadhibu vikali sana watu wa jiji hilo,+ 12 na watu ambao hawakufa walikuwa wamepigwa na bawasiri. Na kilio cha jiji hilo cha kuomba msaada kikapanda mpaka mbinguni.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki