Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 40
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ayubu—Yaliyomo

      • Yehova amuuliza maswali zaidi (1-24)

        • Ayubu akiri hana la kusema (3-5)

        • “Je, utatilia shaka haki yangu?” (8)

        • Mungu aeleza kuhusu nguvu za Behemothi (15-24)

Ayubu 40:2

Marejeo

  • +Ayu 33:12, 13; Isa 45:9
  • +Ayu 13:3; 23:3-5; 31:35

Ayubu 40:4

Marejeo

  • +Ayu 42:5, 6
  • +Zb 39:9; Met 30:32

Ayubu 40:6

Marejeo

  • +Ayu 38:1

Ayubu 40:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “jifunge.”

Marejeo

  • +Ayu 38:3; 42:4

Ayubu 40:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “utabatilisha.”

Marejeo

  • +Zb 51:4; Ro 3:4

Ayubu 40:9

Marejeo

  • +Kut 15:6; Zb 89:13; Isa 40:26; 1Ko 10:22
  • +Ayu 37:4; Zb 29:3

Ayubu 40:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Zifunge nyuso zao.”

Ayubu 40:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nitakapokupongeza.”

Ayubu 40:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Labda ni kiboko.

Ayubu 40:22

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “korongoni.”

Ayubu 40:23

Marejeo

  • +Yos 3:15

Ayubu 40:24

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mtego.”

Jumla

Ayu. 40:2Ayu 33:12, 13; Isa 45:9
Ayu. 40:2Ayu 13:3; 23:3-5; 31:35
Ayu. 40:4Ayu 42:5, 6
Ayu. 40:4Zb 39:9; Met 30:32
Ayu. 40:6Ayu 38:1
Ayu. 40:7Ayu 38:3; 42:4
Ayu. 40:8Zb 51:4; Ro 3:4
Ayu. 40:9Kut 15:6; Zb 89:13; Isa 40:26; 1Ko 10:22
Ayu. 40:9Ayu 37:4; Zb 29:3
Ayu. 40:23Yos 3:15
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ayubu 40:1-24

Ayubu

40 Yehova akaendelea kumjibu Ayubu:

 2 “Je, mtu anayetafuta makosa anapaswa kushindana na Mweza-Yote?+

Acha yule anayetaka kumkaripia Mungu ajibu.”+

3 Ayubu akamjibu Yehova:

 4 “Tazama! Mimi sistahili.+

Nitakujibu nini?

Ninafunika kinywa changu kwa mkono.+

 5 Niliongea mara moja, lakini sitajibu tena;

Mara mbili, lakini sitaongea tena.”

 6 Kisha Yehova akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba ya upepo:+

 7 “Tafadhali, jitayarishe* kama mwanamume;

Nitakuuliza maswali, nawe unijibu.+

 8 Je, utatilia shaka* haki yangu?

Je, utanishutumu ili uwe mwadilifu?+

 9 Je, una mkono wenye nguvu kama mkono wa Mungu wa kweli,+

Au je, sauti yako inaweza kunguruma kama yake?+

10 Tafadhali, jipambe kwa utukufu na ukuu;

Jivike heshima na fahari.

11 Mwaga ghadhabu ya hasira yako;

Mtazame kila mwenye kiburi, umshushe chini.

12 Mtazame kila mwenye kiburi, umnyenyekeze,

Na uwakanyage waovu mahali wanaposimama.

13 Wafiche wote mavumbini;

Wafunge* mahali palipofichika,

14 Ndipo hata mimi nitakapokiri mbele yako*

Kwamba mkono wako wa kulia unaweza kukuokoa.

15 Tazama, huyu ni Behemothi* niliyemuumba kama nilivyokuumba.

Yeye hula majani kama ng’ombe dume.

16 Tazama nguvu zilizo kiunoni mwake

Na nguvu zilizo katika misuli ya tumbo lake!

17 Huukaza mkia wake kama mwerezi;

Kano za mapaja yake zimefumwa pamoja.

18 Mifupa yake ni mabomba ya shaba;

Miguu yake ni kama fito za chuma kilichofuliwa.

19 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu;

Ni Muumba wake tu anayeweza kumkaribia kwa upanga wake.

20 Kwa maana milima huzalisha chakula kwa ajili yake,

Ambako wanyama wote wa mwituni hucheza.

21 Hulala chini ya miti ya miyungiyungi,

Kwenye kivuli cha matete mahali penye umajimaji.

22 Miti ya miyungiyungi humfunika kwa kivuli,

Na mierebi ya bondeni* humzunguka.

23 Mto unaposukasuka, yeye hashtuki.

Haogopi hata maji ya Yordani+ yakifurika kinywani mwake.

24 Je, kuna yeyote anayeweza kumkamata akiwa macho,

Au kumtoboa pua kwa kulabu?*

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki