Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Samweli 8
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

1 Samweli—Yaliyomo

      • Waisraeli wataka mfalme (1-9)

      • Samweli awaonya watu (10-18)

      • Yehova akubali ombi la kutaka mfalme (19-22)

1 Samweli 8:2

Marejeo

  • +1Nya 6:28

1 Samweli 8:3

Marejeo

  • +Kut 18:21
  • +Kut 23:8; Kum 16:19; Zb 15:5; Met 29:4
  • +Kum 24:17

1 Samweli 8:5

Marejeo

  • +Kum 17:14, 15; 1Sa 12:13; Mdo 13:21

1 Samweli 8:7

Marejeo

  • +Amu 8:23; 1Sa 10:19; 12:12; Isa 33:22

1 Samweli 8:8

Marejeo

  • +Kum 9:24
  • +Amu 2:19

1 Samweli 8:11

Marejeo

  • +1Sa 10:25
  • +1Sa 14:52
  • +1Fa 9:22; 10:26
  • +1Fa 4:26

1 Samweli 8:12

Marejeo

  • +2Sa 18:1; 1Nya 27:1
  • +2Fa 1:14
  • +1Nya 27:26
  • +1Fa 4:7
  • +1Fa 4:26

1 Samweli 8:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “wachanganyaji wa manukato.”

Marejeo

  • +1Fa 4:22

1 Samweli 8:14

Marejeo

  • +1Nya 27:28, 31

1 Samweli 8:16

Marejeo

  • +1Fa 5:15, 16

1 Samweli 8:17

Marejeo

  • +1Fa 4:22, 23

1 Samweli 8:18

Marejeo

  • +1Fa 12:3, 4

1 Samweli 8:22

Marejeo

  • +1Sa 8:7; Ho. 13:11

Jumla

1 Sam. 8:21Nya 6:28
1 Sam. 8:3Kut 18:21
1 Sam. 8:3Kut 23:8; Kum 16:19; Zb 15:5; Met 29:4
1 Sam. 8:3Kum 24:17
1 Sam. 8:5Kum 17:14, 15; 1Sa 12:13; Mdo 13:21
1 Sam. 8:7Amu 8:23; 1Sa 10:19; 12:12; Isa 33:22
1 Sam. 8:8Kum 9:24
1 Sam. 8:8Amu 2:19
1 Sam. 8:111Sa 10:25
1 Sam. 8:111Sa 14:52
1 Sam. 8:111Fa 9:22; 10:26
1 Sam. 8:111Fa 4:26
1 Sam. 8:122Sa 18:1; 1Nya 27:1
1 Sam. 8:122Fa 1:14
1 Sam. 8:121Nya 27:26
1 Sam. 8:121Fa 4:7
1 Sam. 8:121Fa 4:26
1 Sam. 8:131Fa 4:22
1 Sam. 8:141Nya 27:28, 31
1 Sam. 8:161Fa 5:15, 16
1 Sam. 8:171Fa 4:22, 23
1 Sam. 8:181Fa 12:3, 4
1 Sam. 8:221Sa 8:7; Ho. 13:11
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
1 Samweli 8:1-22

Kitabu cha Kwanza cha Samweli

8 Samweli alipokuwa amezeeka, aliwaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. 2 Mwana wake wa kwanza aliitwa Yoeli, na wa pili aliitwa Abiya;+ walikuwa waamuzi huko Beer-sheba. 3 Lakini wanawe hawakufuata njia zake; walikuwa na mwelekeo wa kujitafutia faida isiyo ya haki,+ walipokea rushwa,+ na kupotosha haki.+

4 Baada ya muda wazee wote wa Waisraeli walikusanyika pamoja na kuja kumwona Samweli huko Rama. 5 Wakamwambia: “Tazama! Umezeeka, lakini wana wako hawatembei katika njia zako. Basi tuchagulie mfalme awe mwamuzi wetu kama mataifa mengine yote.”+ 6 Lakini Samweli hakufurahi waliposema: “Tupe mfalme awe mwamuzi wetu.” Kwa hiyo Samweli akasali kwa Yehova, 7 Yehova akamwambia Samweli: “Sikiliza mambo yote ambayo watu wanakuambia; kwa maana hawajakukataa wewe, bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.+ 8 Wanatenda kama walivyozoea kutenda tangu nilipowatoa Misri mpaka leo hii; wamekuwa wakiniacha+ na kuabudu miungu mingine,+ na hivyo ndivyo wanavyokutendea wewe pia. 9 Sasa wasikilize. Hata hivyo, unapaswa kuwaonya vikali; waambie mambo ambayo mfalme atakayewatawala atakuwa na haki ya kudai.”

10 Basi Samweli akawaambia maneno yote ya Yehova watu waliokuwa wakimwomba awape mfalme. 11 Akasema: “Mfalme atakayewatawala atakuwa na haki ya kudai mambo haya:+ Atawachukua wana wenu+ na kuwafanya wawe waendeshaji wa magari yake ya farasi+ na wapanda farasi wake,+ na baadhi yao watalazimika kukimbia mbele ya magari yake. 12 Naye atajichagulia wakuu wa maelfu+ na wakuu wa hamsini,+ na baadhi yao watamlimia mashamba yake,+ watavuna mazao yake,+ na kutengeneza silaha zake za vita na vifaa vya magari yake.+ 13 Atachukua mabinti wenu na kuwafanya kuwa watengenezaji wa marashi,* wapishi, na waokaji.+ 14 Atachukua mashamba yenu bora, mashamba yenu bora ya mizabibu, na mashamba yenu bora ya mizeituni+ na kuwapa watumishi wake. 15 Atachukua sehemu ya kumi ya mashamba yenu ya nafaka na mashamba yenu ya mizabibu na kuwapa maofisa wa makao yake na watumishi wake. 16 Naye atachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike, ng’ombe wenu walio bora, na punda wenu na kuwatumia kufanya kazi zake.+ 17 Atachukua sehemu ya kumi ya kondoo wenu na mbuzi wenu,+ nanyi mtakuwa watumishi wake. 18 Siku itafika mtakapolia kwa sababu ya mfalme ambaye mlijichagulia wenyewe,+ lakini Yehova hatawajibu siku hiyo.”

19 Hata hivyo, watu wakakataa kusikiliza mambo ambayo Samweli aliwaambia, wakasema: “Hatutaki, tumeazimia kuwa na mfalme wa kututawala. 20 Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, na mfalme wetu atakuwa mwamuzi wetu, atatuongoza, na kupigana vita vyetu.” 21 Baada ya Samweli kusikia maneno yote ya watu, akayarudia masikioni mwa Yehova. 22 Yehova akamwambia Samweli: “Wasikilize, na uweke mfalme wa kuwatawala.”+ Basi Samweli akawaambia Waisraeli: “Kila mmoja wenu arudi katika jiji lake.”

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki