Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Zekaria 13
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Zekaria—Yaliyomo

      • Sanamu na manabii wa uwongo waondolewa (1-6)

        • Manabii wa uwongo wataaibika (4-6)

      • Mchungaji atapigwa (7-9)

        • Theluthi ya watu kusafishwa (9)

Zekaria 13:1

Marejeo

  • +Eze 36:25, 29

Zekaria 13:2

Marejeo

  • +Kut 23:13
  • +Kum 13:5

Zekaria 13:3

Marejeo

  • +Kum 13:6-9; 18:20

Zekaria 13:4

Marejeo

  • +2Fa 1:8; Mt 3:4

Zekaria 13:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “katikati ya mikono yako.” Yaani, kifuani au mgongoni.

  • *

    Au “wale wanaonipenda.”

Zekaria 13:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kundi la kondoo litawanyike.”

Marejeo

  • +Eze 34:23; Mik 5:4; Yoh 10:11; Ebr 13:20
  • +Isa 53:8; Da 9:26; Mdo 3:18
  • +Mt 26:31, 55, 56; Mk 14:27, 50; Yoh 16:32

Zekaria 13:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “zitakufa.”

Zekaria 13:9

Marejeo

  • +Mal 3:2, 3
  • +Yer 30:22

Jumla

Zek. 13:1Eze 36:25, 29
Zek. 13:2Kut 23:13
Zek. 13:2Kum 13:5
Zek. 13:3Kum 13:6-9; 18:20
Zek. 13:42Fa 1:8; Mt 3:4
Zek. 13:7Eze 34:23; Mik 5:4; Yoh 10:11; Ebr 13:20
Zek. 13:7Isa 53:8; Da 9:26; Mdo 3:18
Zek. 13:7Mt 26:31, 55, 56; Mk 14:27, 50; Yoh 16:32
Zek. 13:9Mal 3:2, 3
Zek. 13:9Yer 30:22
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Zekaria 13:1-9

Zekaria

13 “Siku hiyo kisima kitafunguliwa kwa ajili ya nyumba ya Daudi na wakaaji wa Yerusalemu ili kuwasafisha dhambi na uchafu.+

2 “Siku hiyo,” asema Yehova wa majeshi, “nitafuta majina ya sanamu kutoka nchini,+ nayo hayatakumbukwa tena; nami nitawaondoa kabisa manabii+ na pia roho ya uchafu kutoka nchini. 3 Na mtu akitoa unabii tena, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Hutaishi, kwa sababu umesema uwongo katika jina la Yehova.’ Na baba yake na mama yake waliomzaa watamchoma kisu kwa sababu ya unabii wake.+

4 “Siku hiyo kila nabii ataonea aibu maono yake anapotabiri; nao hawatavaa vazi rasmi la manyoya+ ili kudanganya. 5 Naye atasema, ‘Mimi si nabii. Mimi ni mkulima, kwa sababu mtu fulani alininunua nilipokuwa kijana.’ 6 Na mtu akimuuliza, ‘Majeraha haya uliyo nayo katikati ya mabega yako* yametoka wapi?’ atajibu, ‘Nilijeruhiwa katika nyumba ya rafiki zangu.’”*

 7 “Ee upanga, amka umshambulie mchungaji wangu,+

Mshambulie rafiki yangu,” asema Yehova wa majeshi.

“Mpige mchungaji,+ acha kondoo watawanyike;*+

Nami nitaugeuza mkono wangu dhidi ya watu wa hali ya chini.”

 8 “Na katika nchi yote,” asema Yehova,

“Theluthi mbili za watu zitaangamizwa na kutoweka;*

Na theluthi moja itaachwa humo.

 9 Na theluthi hiyo moja nitaipitisha motoni;

Nami nitawasafisha kama fedha inavyosafishwa,

Na kuwajaribu kama dhahabu inavyojaribiwa.+

Wataliitia jina langu,

Nami nitawajibu.

Nitasema, ‘Wao ni watu wangu,’+

Nao watasema, ‘Yehova ni Mungu wetu.’”

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki