Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 39
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ayubu—Yaliyomo

      • Uumbaji wa wanyama waonyesha ujinga wa mwanadamu (1-30)

        • Mbuzi wa milimani na paa (1-4)

        • Punda mwitu (5-8)

        • Fahali mwitu (9-12)

        • Mbuni (13-18)

        • Farasi (19-25)

        • Kipanga na tai (26-30)

Ayubu 39:1

Marejeo

  • +Zb 104:18
  • +Zb 29:9

Ayubu 39:5

Marejeo

  • +Ayu 24:5; Zb 104:10, 11

Ayubu 39:9

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “katika hori lako.”

Marejeo

  • +Kum 33:17

Ayubu 39:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “alime matuta.”

Ayubu 39:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu zako.”

Ayubu 39:13

Marejeo

  • +Zb 104:17; Zek 5:9

Ayubu 39:16

Marejeo

  • +Omb 4:3

Ayubu 39:17

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “amemfanya asahau.”

Ayubu 39:19

Marejeo

  • +Zb 147:10; Isa 31:1

Ayubu 39:20

Marejeo

  • +Yer 8:16

Ayubu 39:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Huenda kukutana na silaha.”

Marejeo

  • +Amu 5:22; Zb 32:9
  • +Met 21:31; Yer 46:9; 47:3; Hab 1:8

Ayubu 39:22

Marejeo

  • +Isa 5:28; Yer 8:6

Ayubu 39:24

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Humeza ardhi (dunia).”

  • *

    Au labda, “Haamini.”

Ayubu 39:25

Marejeo

  • +Yer 46:4

Ayubu 39:27

Marejeo

  • +Met 23:5; Isa 40:31
  • +Yer 49:16; Oba 4

Ayubu 39:28

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kwenye jino la jabali.”

Ayubu 39:29

Marejeo

  • +Ayu 9:26; Yer 49:22

Ayubu 39:30

Marejeo

  • +Mt 24:28

Jumla

Ayu. 39:1Zb 104:18
Ayu. 39:1Zb 29:9
Ayu. 39:5Ayu 24:5; Zb 104:10, 11
Ayu. 39:9Kum 33:17
Ayu. 39:13Zb 104:17; Zek 5:9
Ayu. 39:16Omb 4:3
Ayu. 39:19Zb 147:10; Isa 31:1
Ayu. 39:20Yer 8:16
Ayu. 39:21Amu 5:22; Zb 32:9
Ayu. 39:21Met 21:31; Yer 46:9; 47:3; Hab 1:8
Ayu. 39:22Isa 5:28; Yer 8:6
Ayu. 39:25Yer 46:4
Ayu. 39:27Met 23:5; Isa 40:31
Ayu. 39:27Yer 49:16; Oba 4
Ayu. 39:29Ayu 9:26; Yer 49:22
Ayu. 39:30Mt 24:28
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ayubu 39:1-30

Ayubu

39 “Je, unajua mbuzi wa milimani huzaa wakati gani?+

Je, umewahi kuwatazama paa wakizaa watoto wao?+

 2 Je, wewe huhesabu miezi ambayo wanabeba mimba?

Je, unajua wakati wanapozaa?

 3 Wao huchuchumaa wanapozaa watoto wao,

Na uchungu wao wa kuzaa huisha.

 4 Watoto wao hupata nguvu na kukua mbugani;

Huenda zao na hawarudi.

 5 Ni nani aliyemwacha huru punda mwitu,+

Na ni nani aliyemfungua kamba punda mwitu?

 6 Nimelifanya jangwa tambarare kuwa makao yake

Na nchi yenye chumvi kuwa makazi yake.

 7 Yeye hudharau vurugu za mji;

Hasikii kelele za mtu anayemwongoza.

 8 Hutangatanga milimani, akitafuta malisho,

Akitafuta mmea wowote wa kijani.

 9 Je, fahali mwitu yuko tayari kukutumikia?+

Je, atalala zizini mwako* usiku?

10 Je, utamfunga fahali mwitu kwa kamba ili alime,

Au, je, atakufuata ili alime* bondeni?

11 Je, utazitumaini nguvu zake nyingi

Na kumwacha afanye kazi zako ngumu?

12 Je, utamtegemea akuletee mavuno yako,*

Na je, atayakusanya kwenye uwanja wako wa kupuria?

13 Mabawa ya mbuni hupigapiga kwa shangwe,

Lakini, je, mabawa na manyoya yake yanaweza kulinganishwa na ya korongo?+

14 Kwa maana yeye huacha mayai yake ardhini,

Na kuyapasha joto mavumbini.

15 Yeye husahau kwamba mguu fulani unaweza kuyavunja

Au kwamba mnyama wa mwituni anaweza kuyakanyaga.

16 Huwatendea wanawe kwa ukatili, kana kwamba si wake;+

Haogopi kwamba huenda kazi yake ngumu ikawa ya bure.

17 Kwa maana Mungu amemnyima* hekima

Naye hajamgawia uelewaji.

18 Lakini anapoinuka na kupigapiga mabawa yake,

Humcheka farasi na yule aliyempanda.

19 Je, ni wewe unayempa farasi nguvu zake?+

Je, unamvika shingoni manyoya marefu yanayotikisika?

20 Je, unaweza kumfanya aruke kama nzige?

Mkoromo wake wa maringo unatisha.+

21 Yeye hukwangua ardhi bondeni na kushangilia kwa nguvu;+

Hukimbia kwenda vitani.*+

22 Huicheka hofu na haogopi chochote.+

Harudi nyuma kwa sababu ya upanga.

23 Podo la mishale hutoa sauti kando yake,

Mkuki na fumo humetameta.

24 Husonga mbele* huku akitetemeka kwa msisimko,

Hawezi kusimama tuli anaposikia* mlio wa pembe.

25 Pembe inapolia, husema, ‘Aha!’

Hunusa vita kutoka mbali sana

Na kusikia kelele za makamanda na kelele za vita.+

26 Je, ni kwa uelewaji wako kwamba kipanga huruka,

Akiyatandaza mabawa yake kuelekea kusini?

27 Au, je, ni kwa agizo lako kwamba tai hupaa juu+

Na kujenga kiota chake juu sana,+

28 Na kulala usiku kucha juu ya jabali,

Akiishi kwenye ngome yake juu ya mwamba uliochongoka?*

29 Akiwa hapo yeye hutafuta chakula;+

Macho yake hutazama mbali sana.

30 Makinda yake hufyonza damu;

Na penye mzoga, ndipo alipo.”+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki