Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 16
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mwanzo—Yaliyomo

      • Hagari na Ishmaeli (1-16)

Mwanzo 16:1

Marejeo

  • +Mwa 15:2, 3
  • +Gal 4:25

Mwanzo 16:2

Marejeo

  • +Mwa 30:1, 3

Mwanzo 16:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “kifuani pako.”

Mwanzo 16:7

Marejeo

  • +Mwa 25:17, 18; Kut 15:22

Mwanzo 16:10

Marejeo

  • +Mwa 17:20; 25:13-16; 1Nya 1:29-31

Mwanzo 16:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Maana yake “Mungu Husikia.”

Mwanzo 16:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Baadhi ya watu hudhani ni pundamilia. Yaelekea ametumiwa kurejelea mtazamo wa kujitegemea.

  • *

    Au labda, “naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.”

Mwanzo 16:13

Marejeo

  • +Met 15:3

Mwanzo 16:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Maana yake “Kisima cha Aliye Hai Ambaye Huniona.”

Mwanzo 16:15

Marejeo

  • +Mwa 21:9; Gal 4:22, 24

Jumla

Mwa. 16:1Mwa 15:2, 3
Mwa. 16:1Gal 4:25
Mwa. 16:2Mwa 30:1, 3
Mwa. 16:7Mwa 25:17, 18; Kut 15:22
Mwa. 16:10Mwa 17:20; 25:13-16; 1Nya 1:29-31
Mwa. 16:13Met 15:3
Mwa. 16:15Mwa 21:9; Gal 4:22, 24
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Mwanzo 16:1-16

Mwanzo

16 Sasa Sarai mke wa Abramu hakuwa amemzalia mtoto yeyote,+ lakini alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Hagari.+ 2 Basi Sarai akamwambia Abramu: “Sasa tafadhali! Yehova amenizuia nisizae watoto. Tafadhali, lala na mtumishi wangu. Huenda nikapata watoto kupitia yeye.”+ Kwa hiyo Abramu akasikiliza maneno ya Sarai. 3 Baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani kwa miaka kumi, Sarai mke wa Abramu akamchukua Hagari, mtumishi wake Mmisri na kumpa Abramu mumewe awe mke wake. 4 Basi Abramu akalala na Hagari, naye akapata mimba. Alipogundua kwamba ana mimba, alianza kumdharau bimkubwa wake.

5 Ndipo Sarai akamwambia Abramu: “Ni wewe uliyesababisha madhara ninayotendewa. Ni mimi niliyemweka mtumishi wangu mikononi mwako,* lakini alipogundua kwamba ana mimba, alianza kunidharau. Yehova na awe mwamuzi kati yangu na wewe.” 6 Basi Abramu akamwambia Sarai: “Tazama! Mtumishi wako yuko chini ya mamlaka yako. Mtendee lolote unaloona ni jema.” Kisha Sarai akamfedhehesha Hagari, naye akamkimbia.

7 Baadaye malaika wa Yehova akamkuta kwenye chemchemi ya maji nyikani, chemchemi iliyo njiani kuelekea Shuri.+ 8 Naye akamuuliza: “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unaenda wapi?” Ndipo akajibu: “Ninamkimbia Sarai, bimkubwa wangu.” 9 Basi malaika wa Yehova akamwambia: “Rudi kwa bimkubwa wako na ujinyenyekeze chini ya mkono wake.” 10 Kisha malaika wa Yehova akasema: “Nitawazidisha sana wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi sana wasiweze kuhesabiwa.”+ 11 Malaika wa Yehova akaendelea kusema: “Sasa una mimba, nawe utazaa mwana, nawe unapaswa kumpa jina Ishmaeli,* kwa maana Yehova amesikia mateso yako. 12 Atakuwa mtu aliye kama pundamwitu.* Mkono wake utapigana na kila mtu, na mkono wa kila mtu utapigana naye, naye atakaa akielekeana na ndugu zake wote.”*

13 Ndipo akaliitia jina la Yehova, aliyekuwa akizungumza naye: “Wewe ni Mungu anayeona,”+ kwa kuwa alisema: “Je, ni kweli kwamba nimemwona hapa yeye ambaye huniona?” 14 Ndiyo sababu kisima hicho kiliitwa Beer-lahai-roi.* (Kiko kati ya Kadeshi na Beredi.) 15 Basi Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwanawe ambaye Hagari alimzaa, Ishmaeli.+ 16 Abramu alikuwa na umri wa miaka 86 Hagari alipomzaa Ishmaeli.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki