Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Isaya 13
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Isaya—Yaliyomo

      • Tangazo dhidi ya Babiloni (1-22)

        • Siku ya Yehova iko karibu! (6)

        • Wamedi kuangusha Babiloni (17)

        • Babiloni halitakaliwa kamwe (20)

Isaya 13:1

Marejeo

  • +Yer 25:12; 50:1-3; Ufu 18:2
  • +Isa 1:1

Isaya 13:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nguzo ya ishara.”

Marejeo

  • +Yer 51:12, 27, 28

Isaya 13:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “watu wangu waliotakaswa.”

Marejeo

  • +Isa 45:1

Isaya 13:4

Marejeo

  • +Da 5:28
  • +Yer 50:15

Isaya 13:5

Marejeo

  • +Yer 50:9; 51:28
  • +Yer 51:11

Isaya 13:6

Marejeo

  • +Isa 13:18; Yer 50:13

Isaya 13:7

Marejeo

  • +Yer 50:43

Isaya 13:8

Marejeo

  • +Da 5:6

Isaya 13:9

Marejeo

  • +Yer 50:23, 29

Isaya 13:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “na Kesili zao,” labda maneno haya yanarejelea kundi la nyota la Orioni na makundi mengine ya nyota yaliyo karibu.

Marejeo

  • +Ayu 9:9; 38:31; Amo 5:8

Isaya 13:11

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “Nitaiwajibisha.”

Marejeo

  • +Zb 137:8; Yer 51:37; Ufu 18:2
  • +Yer 50:29; Da 5:22, 23

Isaya 13:12

Marejeo

  • +Yer 50:30; 51:3, 4
  • +1Fa 10:11

Isaya 13:13

Marejeo

  • +Yer 51:29

Isaya 13:14

Marejeo

  • +Yer 50:16

Isaya 13:15

Marejeo

  • +Yer 51:3, 4

Isaya 13:16

Marejeo

  • +Zb 137:8, 9

Isaya 13:17

Marejeo

  • +Isa 21:2; Yer 50:9; 51:11; Da 5:30, 31

Isaya 13:18

Marejeo

  • +Yer 50:14

Isaya 13:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “pambo la falme.”

Marejeo

  • +Isa 47:5; Da 4:30
  • +Isa 47:1
  • +Mwa 19:24, 25; Yer 50:40

Isaya 13:20

Marejeo

  • +Yer 50:3, 13; 51:29, 37; Ufu 18:21

Isaya 13:21

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “Na roho waovu walio kama mbuzi.”

Marejeo

  • +Ufu 18:2

Isaya 13:22

Marejeo

  • +Yer 51:33

Jumla

Isa. 13:1Yer 25:12; 50:1-3; Ufu 18:2
Isa. 13:1Isa 1:1
Isa. 13:2Yer 51:12, 27, 28
Isa. 13:3Isa 45:1
Isa. 13:4Da 5:28
Isa. 13:4Yer 50:15
Isa. 13:5Yer 50:9; 51:28
Isa. 13:5Yer 51:11
Isa. 13:6Isa 13:18; Yer 50:13
Isa. 13:7Yer 50:43
Isa. 13:8Da 5:6
Isa. 13:9Yer 50:23, 29
Isa. 13:10Ayu 9:9; 38:31; Amo 5:8
Isa. 13:11Zb 137:8; Yer 51:37; Ufu 18:2
Isa. 13:11Yer 50:29; Da 5:22, 23
Isa. 13:12Yer 50:30; 51:3, 4
Isa. 13:121Fa 10:11
Isa. 13:13Yer 51:29
Isa. 13:14Yer 50:16
Isa. 13:15Yer 51:3, 4
Isa. 13:16Zb 137:8, 9
Isa. 13:17Isa 21:2; Yer 50:9; 51:11; Da 5:30, 31
Isa. 13:18Yer 50:14
Isa. 13:19Isa 47:5; Da 4:30
Isa. 13:19Isa 47:1
Isa. 13:19Mwa 19:24, 25; Yer 50:40
Isa. 13:20Yer 50:3, 13; 51:29, 37; Ufu 18:21
Isa. 13:21Ufu 18:2
Isa. 13:22Yer 51:33
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Isaya 13:1-22

Isaya

13 Tangazo dhidi ya Babiloni,+ ambalo Isaya+ mwana wa Amozi aliona katika maono:

 2 “Simamisheni ishara*+ juu ya mlima wa miamba isiyo na kitu.

Wapazieni sauti, wapungieni mkono,

Ili waingie katika milango ya watu wenye vyeo.

 3 Nimewapa amri wale ambao nimewaweka rasmi.*+

Nimewaita mashujaa wangu ili kuonyesha hasira yangu,

Watu wangu wanaoshangilia kwa majivuno.

 4 Sikilizeni! Umati milimani;

Ni kama sauti ya watu wengi sana!

Sikilizeni! Ghasia za falme,

Za mataifa yaliyokusanyika pamoja!+

Yehova wa majeshi anakusanya jeshi kwa ajili ya vita.+

 5 Wanakuja kutoka nchi ya mbali,+

Kutoka mwisho wa mbingu,

Yehova na silaha za ghadhabu yake,

Ili kuiangamiza dunia yote.+

 6 Ombolezeni kwa sauti, kwa maana siku ya Yehova iko karibu!

Itakuja kama maangamizi kutoka kwa Mweza-Yote.+

 7 Ndiyo maana mikono yote italegea,

Na moyo wa kila mwanadamu utayeyuka kwa woga.+

 8 Watu wameshikwa na wasiwasi.+

Wanafurukuta na kushikwa na uchungu,

Kama mwanamke anayezaa.

Wanatazamana kwa hofu,

Wakiwa na nyuso zinazowaka kwa maumivu.

 9 Tazama! Siku ya Yehova inakuja,

Ikiwa na ukali na ghadhabu na hasira inayowaka,

Ili kuifanya nchi iwe kitu cha kutisha,+

Na kuwaangamiza watenda dhambi wa nchi kutoka ndani yake.

10 Kwa maana nyota za mbinguni na makundi yake ya nyota*+

Hazitatoa nuru yake;

Jua litakuwa na giza linapochomoza,

Nao mwezi hautatoa mwanga wake.

11 Nitaiadhibu* dunia inayokaliwa kwa sababu ya ubaya wake,+

Na waovu kwa sababu ya uovu wao.

Nitakikomesha kiburi cha wenye kimbelembele,

Nami nitayashusha majivuno ya waonevu.+

12 Nitamfanya mwanadamu anayeweza kufa kuwa haba kuliko dhahabu safi,+

Na wanadamu kuwa haba kuliko dhahabu ya Ofiri.+

13 Ndiyo maana nitazifanya mbingu zitetemeke

Na dunia itatikiswa itoke mahali pake+

Kwa sababu ya ghadhabu ya Yehova wa majeshi katika siku ya hasira yake inayowaka.

14 Kama swala anayewindwa na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya

Kila mtu atarudi kwa watu wake mwenyewe;

Kila mtu atakimbilia nchi yake mwenyewe.+

15 Yeyote atakayepatikana atachomwa kwa silaha,

Na yeyote atakayekamatwa atauawa kwa upanga.+

16 Watoto wao watavunjwa vipandevipande mbele ya macho yao,+

Nyumba zao zitaporwa,

Na wake zao watabakwa.

17 Tazama, ninawainua Wamedi dhidi yao,+

Ambao hawaioni fedha kuwa kitu

Na ambao hawapendezwi na dhahabu.

18 Pinde zao zitawavunjavunja vijana;+

Hawatausikitikia uzao wa tumbo

Wala kuwahurumia watoto.

19 Na Babiloni, ufalme wenye utukufu zaidi,*+

Uzuri na fahari ya Wakaldayo,+

Litakuwa kama Sodoma na Gomora yalipoangamizwa na Mungu.+

20 Halitakaliwa kamwe,

Wala halitakuwa makao ya watu kwa vizazi vyote.+

Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko,

Na hakuna wachungaji watakaopumzisha mifugo yao huko.

21 Viumbe wa jangwani watalala huko;

Nyumba zao zitajaa bundi-tai.

Mbuni watakaa huko,+

Mbuzi wa mwituni* watarukaruka huko.

22 Wanyama wanaopiga mayowe watalia kwa sauti katika minara yake,

Na mbwamwitu katika majumba yake ya kifahari.

Wakati wake umekaribia, na siku zake hazitarefushwa.”+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki