Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 13
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mwanzo—Yaliyomo

      • Abramu arudi Kanaani (1-4)

      • Abramu na Loti watengana (5-13)

      • Mungu arudia ahadi aliyompa Abramu (14-18)

Mwanzo 13:1

Marejeo

  • +Mwa 12:9; 20:1

Mwanzo 13:2

Marejeo

  • +Mwa 24:34, 35

Mwanzo 13:3

Marejeo

  • +Mwa 12:8, 9; Yos 7:2

Mwanzo 13:7

Marejeo

  • +Mwa 10:19

Mwanzo 13:8

Marejeo

  • +Mwa 11:27

Mwanzo 13:10

Marejeo

  • +Mwa 19:28
  • +Mwa 2:8, 9
  • +Mwa 19:20-22

Mwanzo 13:12

Marejeo

  • +Mwa 19:28, 29

Mwanzo 13:13

Marejeo

  • +Mwa 18:20; 19:5; 2Pe 2:6-8; Yud 7

Mwanzo 13:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yako.”

Marejeo

  • +Mwa 12:7; 15:18; 24:7; Kut 33:1

Mwanzo 13:16

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “nitaifanya mbegu yako iwe.”

  • *

    Tnn., “mbegu yako itaweza.”

Marejeo

  • +Mwa 12:2; 15:1, 5; Kut 1:7; Ebr 11:12

Mwanzo 13:18

Marejeo

  • +Mwa 18:1; 23:19; 25:9, 10; 35:27
  • +Mwa 23:2
  • +Mwa 12:7

Jumla

Mwa. 13:1Mwa 12:9; 20:1
Mwa. 13:2Mwa 24:34, 35
Mwa. 13:3Mwa 12:8, 9; Yos 7:2
Mwa. 13:7Mwa 10:19
Mwa. 13:8Mwa 11:27
Mwa. 13:10Mwa 19:28
Mwa. 13:10Mwa 2:8, 9
Mwa. 13:10Mwa 19:20-22
Mwa. 13:12Mwa 19:28, 29
Mwa. 13:13Mwa 18:20; 19:5; 2Pe 2:6-8; Yud 7
Mwa. 13:15Mwa 12:7; 15:18; 24:7; Kut 33:1
Mwa. 13:16Mwa 12:2; 15:1, 5; Kut 1:7; Ebr 11:12
Mwa. 13:18Mwa 18:1; 23:19; 25:9, 10; 35:27
Mwa. 13:18Mwa 23:2
Mwa. 13:18Mwa 12:7
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Mwanzo 13:1-18

Mwanzo

13 Kisha Abramu akapanda kutoka Misri kwenda Negebu,+ yeye pamoja na mke wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, pamoja na Loti. 2 Abramu alikuwa na utajiri mwingi wa mifugo, fedha, na dhahabu.+ 3 Alipiga kambi sehemu moja baada ya nyingine aliposafiri kutoka Negebu kwenda Betheli, mpaka alipofika mahali alipokuwa amepiga hema lake kati ya Betheli na Ai,+ 4 mahali alipokuwa amejenga madhabahu mwanzoni. Huko, Abramu akaliitia jina la Yehova.

5 Sasa Loti, aliyekuwa akisafiri pamoja na Abramu, alikuwa pia na kondoo, ng’ombe, na mahema. 6 Basi wote hawangeweza kukaa pamoja kwa sababu nchi haikuwatosha; mali zao zilikuwa zimeongezeka sana hivi kwamba hawangeweza tena kukaa pamoja. 7 Kwa sababu hiyo, ugomvi ukatokea kati ya wachungaji wa mifugo ya Abramu na wachungaji wa mifugo ya Loti. (Wakati huo Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi hiyo.)+ 8 Basi Abramu akamwambia Loti:+ “Tafadhali, pasiwe na ugomvi wowote kati yangu mimi na wewe na kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako, kwa maana sisi ni ndugu. 9 Je, nchi yote haiko mbele yako? Tafadhali, jitenge nami. Ukienda kushoto, nitakwenda kulia; lakini ukienda kulia, basi mimi nitakwenda kushoto.” 10 Kwa hiyo Loti akainua macho yake na kuona kwamba wilaya yote ya Yordani+ ilikuwa na maji ya kutosha (kabla Yehova hajaharibu Sodoma na Gomora), kama bustani ya Yehova,+ kama nchi ya Misri, mpaka Soari.+ 11 Basi Loti akajichagulia wilaya yote ya Yordani, naye Loti akahamisha kambi yake kuelekea upande wa mashariki. Kwa hiyo wakatengana. 12 Abramu aliishi katika nchi ya Kanaani, lakini Loti aliishi katika majiji ya wilaya hiyo.+ Hatimaye akapiga hema lake karibu na Sodoma. 13 Sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu, nao walitenda dhambi nzito machoni pa Yehova.+

14 Yehova akamwambia hivi Abramu baada ya Loti kujitenga naye: “Tafadhali, inua macho yako, na kutoka mahali ulipo tazama kaskazini na kusini, mashariki na magharibi, 15 kwa sababu nchi yote unayoona, nitakupa wewe na uzao wako* iwe miliki yenu ya kudumu.+ 16 Nami nitaufanya uzao wako uwe* kama chembe za mavumbi ya ardhi, hivi kwamba ikiwa kuna yeyote anayeweza kuhesabu chembe za mavumbi ya ardhi, basi uzao wako utaweza* kuhesabiwa.+ 17 Ondoka, safiri kwa mapana na marefu katika nchi hii, kwa maana nitakupa wewe nchi hii.” 18 Basi Abramu akaendelea kuishi katika mahema. Baadaye akaja na kuishi kati ya miti mikubwa ya Mamre,+ ambayo iko Hebroni,+ na huko akamjengea Yehova madhabahu.+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki