Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb 5
  • Safina ya Noa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Safina ya Noa
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Gharika Kubwa​—Nani Alimsikiliza Mungu? Nani Hakumsikiliza?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb 5
Noa na familia yake wakijenga safina

SOMO LA 5

Safina ya Noa

Watu walizidi kuongezeka duniani na wengi walikuwa wakifanya mambo mabaya. Hata baadhi ya malaika wa mbinguni wakawa wabaya. Waliacha makao yao huko mbinguni na kuja duniani. Je, unajua ni kwa nini walifanya hivyo? Ili wavae miili ya wanadamu na kujichukulia wanawake.

Malaika walijichukulia wanawake na kuzaa watoto. Watoto hao walikuwa watu wenye nguvu sana na wajeuri. Waliwapiga watu. Yehova hangeruhusu hali hiyo iendelee. Hivyo aliamua kuwaharibu watu wabaya kupitia gharika.

Noa na familia yake wakijenga safina

Lakini kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa tofauti na watu hao. Alimpenda Yehova. Jina lake ni Noa. Alikuwa na mke na watoto watatu, yaani, Shemu, Hamu, na Yafethi, na kila mtoto alikuwa na mke. Yehova alimwambia Noa atengeneze safina, ili yeye na familia yake waokoke Gharika. Safina ilikuwa sanduku kubwa lililoelea majini. Pia, Yehova alimwambia Noa awaingize wanyama ndani ya safina ili wao pia waokoke.

Mara moja, Noa alianza kujenga safina. Noa na familia yake walijenga safina kwa karibu miaka 50. Walitengeneza safina kulingana na maagizo ya Yehova. Katika kipindi hicho, Noa aliwaonya watu kuhusu Gharika. Hata hivyo, watu hawakumsikiliza.

Hatimaye, muda wa kuingia ndani ya safina ukafika. Acha tuone kile kilichotokea baadaye.

“Kama siku za Noa zilivyokuwa, ndivyo kuwapo kwa Mwana wa binadamu kutakavyokuwa.”​—Mathayo 24:37

Maswali: Kwa nini Yehova alileta Gharika? Yehova alimpa Noa maagizo gani?

Mwanzo 6:1-22; Mathayo 24:37-41; 2 Petro 2:5; Yuda 6

    Tanzanian sign language publications(2020-2025)
    Toka
    Ingia
    • Lugha ya Alama ya Tanzania
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki