-
2 Wafalme 11:19, 20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Tena, akawachukua wakuu wa mamia,+ walinzi walioitwa Wakari, walinzi wa jumba la mfalme,+ na watu wote nchini ili wamsindikize mfalme kushuka kutoka katika nyumba ya Yehova, wakaja katika jumba la mfalme kupitia lango la walinzi wa jumba la mfalme. Kisha mfalme akaketi kwenye kiti cha wafalme.+ 20 Basi watu wote nchini wakashangilia na jiji likatulia, kwa maana walikuwa wamemuua Athalia kwa upanga katika jumba la mfalme.
-