-
1 Samweli 22:17, 18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
17 Ndipo mfalme akawaambia walinzi* waliomzunguka: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Yehova, kwa sababu wamemuunga mkono Daudi! Walijua kwamba ametoroka, lakini hawakunijulisha!” Lakini watumishi hao wa mfalme hawakutaka kuinua mikono yao wawashambulie makuhani wa Yehova. 18 Basi mfalme akamwambia Doegi:+ “Wewe geuka uwashambulie makuhani!” Mara moja Doegi Mwedomu+ akageuka na kuwashambulia hao makuhani yeye mwenyewe. Siku hiyo aliwaua wanaume 85 waliovaa efodi ya kitani.+
-
-
1 Wafalme 2:29Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
29 Kisha Mfalme Sulemani akaambiwa hivi: “Yoabu amekimbilia katika hema la Yehova, na yuko humo kando ya madhabahu.” Kwa hiyo Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema: “Nenda ukamuue!”
-