-
Mathayo 21:28-31Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
28 “Mnaonaje? Mtu fulani alikuwa na watoto wawili. Akamwendea wa kwanza, akamwambia, ‘Mwanangu, leo nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu.’ 29 Akamjibu, ‘Sitaenda,’ lakini baadaye akajuta na akaenda. 30 Akamwendea wa pili na kumwambia jambo hilohilo. Naye akamjibu, ‘Nitaenda Baba,’ lakini hakwenda. 31 Kati ya hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake?” Wakasema: “Yule wa kwanza.” Yesu akasema: “Kwa kweli ninawaambia wakusanya kodi na makahaba wanawatangulia ninyi kuingia katika Ufalme wa Mungu.
-