-
Mathayo 26:47-50Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
47 Alipokuwa bado akizungumza, tazama! Yuda, mmoja wa wale 12, akaja pamoja na umati mkubwa wakiwa na mapanga na marungu, walikuwa wametumwa na wakuu wa makuhani na wazee wa watu.+
48 Basi msaliti wake alikuwa amewapa ishara, akisema: “Yule nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.” 49 Akaenda moja kwa moja kwa Yesu akasema: “Salamu, Rabi!” kisha akambusu kwa wororo. 50 Lakini Yesu akamuuliza: “Mwenzangu, umekuja kufanya nini?”+ Ndipo wakaja na kumkamata Yesu na kumtia nguvuni.
-
-
Marko 14:43-46Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
43 Na mara moja, alipokuwa bado akizungumza, Yuda, mmoja wa wale 12, akafika pamoja na umati wenye mapanga na marungu, walikuwa wametumwa na wakuu wa makuhani, waandishi, na wazee.+ 44 Basi msaliti wake alikuwa amewapa ishara waliyokubaliana akisema: “Yule nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni na kuondoka naye akiwa chini ya ulinzi.” 45 Akaja moja kwa moja akamkaribia na kusema, “Rabi!” kisha akambusu kwa wororo. 46 Basi wakamkamata na kumtia nguvuni.
-