Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya Methali—Yaliyomo METHALI YALIYOMO 1 Kusudi la methali (1-7) Hatari za marafiki wabaya (8-19) Hekima ya kweli hupaza sauti hadharani (20-33) 2 Thamani ya hekima (1-22) Tafuta hekima kama hazina zilizofichika (4) Uwezo wa kufikiri ni ulinzi (11) Uasherati huleta msiba (16-19) 3 Uwe na hekima na umtumaini Yehova (1-12) Mheshimu Yehova kwa vitu vyenye thamani (9) Hekima huleta furaha (13-18) Hekima huleta usalama (19-26) Mambo mema ya kuwatendea wengine (27-35) Watendee wengine mema inapowezekana (27) 4 Mafundisho ya baba yenye hekima (1-27) Zaidi ya yote, pata hekima (7) Epuka vijia vya uovu (14, 15) Kijia cha waadilifu huzidi kung’aa (18) “Ulinde moyo wako” (23) 5 Onyo dhidi ya wanawake waasherati (1-14) Shangilia pamoja na mke wako (15-23) 6 Jihadhari kuhusiana na kutoa dhamana ya mkopo (1-5) “Mwendee chungu, ewe mvivu” (6-11) Mtu mwovu asiyefaa kitu (12-15) Vitu saba ambavyo Yehova anachukia (16-19) Jilinde dhidi ya mwanamke mwovu (20-35) 7 Zishike amri za Mungu uishi (1-5) Kijana mjinga atongozwa (6-27) “Kama ng’ombe dume anayeenda machinjioni” (22) 8 Hekima yaongea kama mtu (1-36) ‘Mimi ni mwanzo kabisa wa kazi za Mungu’ (22) ‘Nilikuwa kando ya Mungu nikiwa mfanyakazi stadi’ (30) “Niliwapenda sana wanadamu” (31) 9 Hekima ya kweli inatoa mwaliko (1-12) “Nitafanya siku zako ziwe nyingi” (11) Mwanamke mpumbavu awaalika watu (13-18) “Maji yaliyoibwa ni matamu” (17) METHALI ZA SULEMANI (10:1–24:34) 10 Mwana mwenye hekima humfanya baba yake ashangilie (1) Mikono yenye bidii huleta utajiri (4) Kusema maneno mengi husababisha makosa (19) Baraka ya Yehova hutajirisha (22) Kumwogopa Yehova hurefusha maisha (27) 11 Wenye kiasi wana hekima (2) Mwasi imani huwaangamiza wengine (9) “Washauri wengi huleta mafanikio” (14) Mtu mkarimu atapata ufanisi (25) Anayeutumaini utajiri wake ataanguka (28) 12 Anayechukia karipio hana akili (1) “Maneno yanayosemwa bila kufikiri huchoma kama upanga” (18) Kusitawisha amani huleta shangwe (20) Midomo inayosema uwongo humchukiza Yehova (22) Mahangaiko huulemea moyo (25) 13 Wanaotafuta ushauri wana hekima (10) Tumaini likikawia huufanya moyo uwe mgonjwa (12) Mjumbe mwaminifu huleta maponyo (17) Kutembea na wenye hekima humfanya mtu awe na hekima (20) Nidhamu huonyesha upendo (24) 14 Moyo hujua uchungu wake wenyewe (10) Njia inayoonekana kuwa sawa inaweza kusababisha kifo (12) Mjinga huamini kila neno (15) Tajiri ana marafiki wengi (20) Moyo mtulivu huupa mwili uzima (30) 15 Jibu la upole hutuliza hasira (1) Macho ya Yehova yako kila mahali (3) Sala ya mtu mnyoofu humfurahisha Mungu (8) Mipango huvunjika watu wasiposhauriana (22) Tafakari kabla ya kujibu (28) 16 Yehova huchunguza nia (2) Mkabidhi Yehova kazi zako (3) Mizani ya unyoofu hutoka kwa Yehova (11) Kiburi hutangulia kuanguka kwa kishindo (18) Mvi ni taji la umaridadi (31) 17 Usilipe uovu kwa wema (13) Ondoka kabla ugomvi haujaanza (14) Rafiki wa kweli hupenda nyakati zote (17) “Moyo wenye shangwe ni dawa nzuri” (22) Mtu mwenye utambuzi huyazuia maneno yake (27) 18 Kujitenga na wengine ni jambo la kichoyo lisilo la hekima (1) Jina la Yehova ni mnara wenye nguvu (10) Mali ni ulinzi wa kuwaziwa tu (11) Hekima ya kusikiliza pande zote mbili (17) Rafiki hushikamana na mtu kwa ukaribu kuliko ndugu (24) 19 Ufahamu hutuliza hasira (11) Mke mgomvi ni kama paa linalovuja (13) Mke mwenye busara hutoka kwa Yehova (14) Mtie mtoto nidhamu wakati bado kuna tumaini (18) Hekima ya kusikiliza mashauri (20) 20 Divai ni mdhihaki (1) Mvivu halimi katika majira ya baridi kali (4) Mawazo ya mtu ni kama maji yenye kina (5) Onyo dhidi ya kuapa haraka-haraka (25) Utukufu wa vijana ni nguvu zao (29) 21 Yehova huuelekeza moyo wa mfalme (1) Haki ni bora kuliko dhabihu (3) Bidii huleta mafanikio (5) Asiyemsikiliza mtu wa hali ya chini hatasikilizwa (13) Hakuna hekima katika kumpinga Yehova (30) 22 Jina jema ni bora kuliko mali nyingi (1) Mazoezi ya mapema ya mtoto yatadumu maisha yake yote (6) Mvivu huogopa kwamba simba yuko nje (13) Nidhamu huondoa ujinga (15) Mfanyakazi stadi huwatumikia wafalme (29) 23 Uwe na busara unapokubali mwaliko (2) Usifuatie utajiri (4) Utajiri unaweza kuruka mbali nawe (5) Usiwe miongoni mwa walevi (20) Kileo huuma kama nyoka (32) 24 Usiwaonee wivu waovu (1) Nyumba hujengwa kwa hekima (3) Mwadilifu anaweza kuanguka lakini atainuka (16) Usilipize kisasi (29) Kusinzia huleta umaskini (33, 34) METHALI ZA SULEMANI ZILIZONAKILIWA NA WATU WA MFALME HEZEKIA (25:1–29:27) 25 Kutunza siri (9) Maneno yaliyochaguliwa vizuri (11) Kuheshimu faragha ya wengine (17) Kukusanya makaa ya mawe juu ya kichwa cha adui (21, 22) Habari njema ni kama maji baridi (25) 26 Ufafanuzi kuwahusu watu wavivu (13-16) Epuka ugomvi usiokuhusu (17) Epuka mizaha inayodhuru (18, 19) Pasipo na kuni, moto huzimika (20, 21) Maneno ya mchongezi ni kama matonge matamu (22) 27 Karipio kutoka kwa rafiki hunufaisha (5, 6) Mwanangu, ufanye moyo wangu ushangilie (11) Chuma hunoa chuma (17) Lijue kundi lako (23) Mali haidumu milele (24) 28 Sala ya mtu asiyesikiliza inachukiza (9) Anayeungama huonyeshwa rehema (13) Anayeharakisha kupata utajiri hatakosa hatia (20) Karipio ni bora kuliko kusifusifu (23) Mtu mkarimu hakosi chochote (27) 29 Mtoto aliyeachiliwa huleta aibu (15) Bila maono, watu hutenda wapendavyo (18) Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi (22) Mtu mnyenyekevu hupata utukufu (23) Kuwaogopa wanadamu ni mtego (25) 30 MANENO YA AGURI (1-33) Usinipe umaskini wala utajiri (8) Vitu visivyotosheka kamwe (15, 16) Vitu visivyoacha alama (18, 19) Mwanamke mzinzi (20) Wanyama wenye hekima ya kisilika (24) 31 MANENO YA MFALME LEMUELI (1-31) Ni nani anayeweza kumpata mke mwema? (10) Hufanya kazi kwa bidii na jitihada (17) Fadhili ziko kwenye ulimi wake (26) Watoto wake na mume wake humsifu (28) Sura nzuri na urembo hutoweka upesi (30)