Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/22 uku. 32
  • Dawa ya Matatizo ya Ubaguzi wa Rangi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Dawa ya Matatizo ya Ubaguzi wa Rangi
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 9/22 uku. 32

Dawa ya Matatizo ya Ubaguzi wa Rangi

Hivi majuzi mwanamume mmoja kutoka Oklahoma, Marekani, alipokea nakala ya gazeti Amkeni! iliyokazia habari “Je! Jamii Zote Zitapata Kuungana Wakati Wowote?” Akielekeza barua yake kwa “Wachapishaji Wapendwa wa Mnara wa Mlinzi,” mtu huyo aliandika hivi:

“Sasa hivi nimepata fursa njema kusoma toleo lenu la Agosti 22, 1993 la Amkeni! linaloshughulika na tatizo la mahusiano ya watu wa rangi mbalimbali. Niligutushwa, na kuvutiwa, na uelewevu wenu wa maoni yasiyopendelea na yenye ufahamu wa kina kirefu juu ya tatizo gumu hili.

“Hivi majuzi nilimaliza mtaala wa koleji kuhusu historia ya Marekani. Lakini katika kurasa 9 tu za gazeti lenu mlitoa historia fupi yenye kueleweka, elezo, NA DAWA juu ya tatizo hili lisiloeleweka wazi lizidilo muhula mzima wa kuandika habari na kusikia mihadhara kwenye koleji. Makala hizo zilikuwa na usawaziko sana hata haiwezekani kujua waandikaji ni wa malezi ya rangi gani.

“Ulimwengu uzidipo kuegemea upande mmoja tu wa kikabila, kila mtu ahitaji kuwekewa wazi habari za aina hii, kwa wingi kadiri mwezavyo kuzichapisha. Asanteni kwa kuwa na moyo mkuu kuchapisha kweli na mambo ya utimamu.”

Ikiwa ungependa nakala ya Amkeni! ipelekwe nyumbani kwako, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki