Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ingawa huenda wengine “wakageuzia mbali masikio yao kuacha kweli,” Timotheo alionywa kwa upole afanye nini? (2 Timotheo 4:4, 5)
2. Ni nani waliokuwa wasimamizi wawili wa nyumba ya mfalme ambao walifanya njama dhidi ya Mfalme Ahasuero? (Esta 2:21)
3. Nimrodi alijipatia sifa ya kuwa nani? (Mwanzo 10:9)
4. Ni nani aliyekuwa mke wa pili wa Abrahamu? (Mwanzo 25:1)
5. Yesu alimponya jinsi gani mwanamke “aliyeshikwa na mtiririko wa damu miaka kumi na miwili”? (Marko 5:27-29)
6. Akitoa kielezi cha jinsi ingekuwa vigumu “kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu,” Yesu alisema ni nini ingekuwa rahisi zaidi? (Luka 18:25)
7. Ni uhakikisho upi wa kisheria ambao Mungu alitumia kutoa uhakikisho wa ziada kwa ahadi yake? (Waebrania 6:17)
8. Ni sehemu ipi ya sanamu ya ndoto ya Nebukadreza iliyofanyizwa kwa chuma na udongo wa mfinyanzi? (Danieli 2:41, 42)
9. Ni mmea upi ambao Waisraeli walitumia kupaka damu juu ya miimo ya milango yao ili kwamba malaika wa Mungu ahifadhi wazaliwa wao wa kwanza? (Kutoka 12:22)
10. Ni mnyama yupi aliyetumiwa hasa katika shughuli za vita nyakati za kale? (Kutoka 15:21)
11. Ni nini ambayo Maandiko husema kwamba Yehova hawezi kufanya? (Waebrania 6:18)
12. Ni wapi ambapo Yehova alimwagiza Eliya ajifiche na kulishwa na kunguru? (1 Wafalme 17:3)
13. Yehova aliwapa nani mgawo wa kulibeba sanduku la agano? (Kumbukumbu la Torati 10:8)
14. Ni nani ambaye Paulo alimtaja kuwa “mchaguliwa katika Bwana”? (Waroma 16:13)
15. Ni nani aliyekuwa baba ya Shekemu, ambaye pia aliuawa baada ya Shekemu kumnajisi Dina? (Mwanzo 34:26)
16. Ni nani aliyekuwa baba ya Abrahamu? (Yoshua 24:2)
17. Ni nini ambacho Mungu alitaka kilipwe ili kufidia wazaliwa wa kwanza 273 wa makabila mengine waliowazidi Walawi? (Hesabu 3:46, 47)
18. Mtumwa Mwisraeli angewekwa huru ikiwa sehemu zipi za mwili wake zingeharibiwa na bwana-mkubwa wake? (Kutoka 21:26, 27)19. Ni nini ambayo Yesualisema ingemweka mtu huru? (Yohana 8:32)
20. Kwa sababu ya upendano vilevile usawa wa daraja na cheo, Mfalme Hiramu alimwitaje Solomoni? (1 Wafalme 9:13)
21. Ni mti upi unaotajwa tu katika kitabu cha Wimbo Ulio Bora, ambao ulithaminiwa kwa harufu yake nzuri na uliotumika kuwa kipodozi? (Wimbo Ulio Bora 1:14)
22. Ni nani waliopoteza maisha yao baba yao alipojenga upya Yeriko, kwa utimizo wa laana ya Yoshua? (1 Wafalme 16:34)
23. Ni kitu gani kilichoifanya safina ya Noa isipenye maji? (Mwanzo 6:14)
[Sanduku katika ukurasa wa 27]
Majibu ya Maswali
1. ‘Atunze akili zake katika mambo yote, avumilie uovu, afanye kazi ya mweneza-evanjeli, atimize kikamili huduma yake’
2. Bigthani na Tereshi
3. “Hodari [wa] kuwinda wanyama mbele za BWANA”
4. Ketura
5. Aligusa vazi lake la nje
6. “Kwa ngamia kupita katika tundu la sindano ya kushonea”
7. Kiapo
8. Nyayo za miguu na vidole
9. Hisopo
10. Farasi
11. Uwongo
12. Kijito cha Kerithi
13. Kabila la Lawi
14. Rufo
15. Hamori
16. Tera
17. Bei ya fidia ya shekeli tano kwa kila mmoja
18. Jicho au jino
19. Kujua kweli
20. Ndugu
21. Hina
22. Abiramu na Segubu
23. Lami