Yathaminiwa na Daktari wa Kitiba
Daktari mmoja wa kitiba katika Frankfurt, Ujeremani ya Magharibi, ambaye alikuwa amealikwa afanye upya maandikisho yake ya magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! si kwamba tu alipeleka pesa za kuyaandikisha upya, bali pia alieleza:
“Mimi nastaajabu daima kupata toleo pana hivyo la makala zilizo nzuri kweli kweli na za kupendeza sana—nyingi zazo zikiwa na habari zisizohusiana na dini—kwa bei ya chini sana. Ingawa mimi nina wakati mchache kwa ajili yangu binafsi, mara nyingi nilitumia jioni zangu nikiwa nimejikunja katika sebule la nyumba yangu kusoma magazeti yenu karibu na taa. Kwa mara nyingine, asanteni kwa jitihada zenu.”
Kwa nini usifurahie kujisomea mwenyewe habari hizi zilizo bora? Unaweza kupata majarida haya mawili yenye thamani kubwa kwa kujaza na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini.
Tafadhali mnipelekee andikisho la mwaka mmoja la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mimi nawapelekea Kshs. 97/- (Tshs. 360/-).