Maelezo ya Chini
b Kila moja ya sarafu hizi ilikuwa leptoni, sarafu ndogo zaidi ya Kiyahudi iliyotumiwa wakati huo. Lepta mbili (moja ni leptoni, nyingi ni lepta) zilitoshana na sehemu moja ya 64 ya mshahara wa siku. Kulingana na Mathayo 10:29, kuwa na sarafu ya asarioni (inayolingana na lepta nane), mtu angeweza kununua shomoro wawili ambao walikuwa miongoni mwa ndege wa bei ya chini zaidi waliotumiwa kwa chakula na maskini. Kwa hiyo mjane huyo alikuwa maskini kwelikweli, kwa kuwa alikuwa na nusu tu ya kiasi cha kununua shomoro mmoja, ambacho hakingeweza kutosha hata mlo mmoja.