-
Abrahamu—Kielelezo cha ImaniMnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
Kulingana na Mwanzo 11:31, Abramu aliishi na familia yake katika mji wenye ufanisi wa “Uru wa Wakaldayo,” ambao wakati mmoja ulikuwa mashariki ya Mto Eufrati.a Hivyo, hakukua akiwa mhamaji mwenye kuishi mahemani bali alikuwa mkazi wa mji wenye anasa nyingi. Bidhaa kutoka nchi za nje zingeweza kununuliwa kwenye masoko ya Uru. Mitaa ya Uru ilikuwa na nyumba kubwa zilizopakwa chokaa ambazo zilikuwa na maji ya mfereji.
4. (a) Ni magumu gani ambayo waabudu wa Mungu wa kweli walipata huko Uru? (b) Abramu alikuja kudhihirishaje imani katika Yehova?
4 Mbali na manufaa za kimwili, maisha katika mji wa Uru yalifanya hali iwe ngumu sana kwa mtu yeyote aliyetaka kumtumikia Mungu wa kweli. Mji huo ulikolea ibada ya sanamu na ushirikina. Naam, jengo lililokuwa kubwa zaidi mjini humo ni hekalu refu lililomtukuza mungu-mwezi aitwaye Nanna. Yaelekea Abramu alishinikizwa sana, hata na watu fulani wa jamaa yake ashiriki ibada hiyo iliyopotoka. Kulingana na mapokeo fulani ya Wayahudi, Tera babake Abramu alikuwa mtengeneza sanamu. (Yoshua 24:2, 14, 15) Kwa vyovyote vile, Abramu hakushiriki ibada isiyo ya kweli na iliyopotoka. Babu yake Shemu aliyekuwa mzee alikuwa bado hai na yaelekea alimwambia Abramu kuhusu Mungu wa kweli. Kwa sababu hiyo, Abramu alidhihirisha imani katika Yehova badala ya Nanna!—Wagalatia 3:6.
-
-
Abrahamu—Kielelezo cha ImaniMnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
8. Imani ya Abramu ilikuwa na matokeo gani kwa washiriki wa karibu wa familia yake, nao Wakristo wanaweza kujifunza nini kutokana na jambo hilo?
8 Vipi washiriki wa karibu wa familia ya Abramu? Yaelekea imani na usadikisho wa Abramu ulikuwa na matokeo yenye kutokeza kwa familia yake, kwa kuwa Sarai mke wake na mpwa wake Loti, aliyekuwa yatima, walichochewa kutii amri ya Mungu ya kuondoka Uru. Nahori, nduguye Abramu, na baadhi ya wazao wake waliondoka Uru baadaye, wakawa wakazi wa Harani ambako walimwabudu Yehova. (Mwanzo 24:1-4, 10, 31; 27:43; 29:4, 5) Hata Tera babake Abramu alikubali kuondoka pamoja na mwanawe! Hivyo, Biblia inasema kwamba Tera, akiwa kichwa cha familia, ndiye aliyechukua hatua ya kuhamisha familia yake kwenda Kanaani. (Mwanzo 11:31) Sisi pia tunaweza kufurahia mafanikio ya kadiri fulani tukiwatolea jamaa zetu ushahidi kwa busara.
9. Ilimpasa Abramu afanye matayarisho gani kwa ajili ya safari yake, na kwa nini huenda matayarisho hayo yalitia ndani kujidhabihu?
9 Kabla ya kuanza safari yake, Abramu alikuwa na shughuli nyingi. Ilimpasa kuuza mali na bidhaa na kununua mahema, ngamia, chakula, na vifaa alivyohitaji. Huenda Abramu alipata hasara kwa sababu ya matayarisho hayo ya harakaharaka, lakini alifurahia kumtii Yehova. Ilikuwa siku muhimu kama nini wakati alipomaliza matayarisho hayo na msafara wake ukasimama nje ya kuta za Uru, ukiwa tayari kusafiri! Msafara huo ulisafiri kuelekea kaskazini-magharibi, kandokando ya sehemu iliyojipinda ya Mto Eufrati. Baada ya kusafiri umbali upatao kilometa 1,000 kwa majuma kadhaa, msafara huo ulifika kwenye mji uliokuwa kaskazini mwa Mesopotamia uitwao Harani, kituo kikuu cha misafara.
10, 11. (a) Yaelekea ni kwa nini Abramu alikaa Harani kwa muda fulani? (b) Wakristo wanaowatunza wazazi wao wazee wanapewa kitia moyo gani?
10 Yaelekea Abramu alikaa Harani kwa sababu ya babake Tera, aliyekuwa mzee. (Mambo ya Walawi 19:32) Vivyo hivyo Wakristo wengi leo wana pendeleo la kutunza wazazi wao wazee au wagonjwa, wengi hata wakifanya marekebisho fulani ili kufanya hivyo. Inapokuwa lazima kuwatunza wazazi, watu hao wanaweza kuwa na hakika kwamba kujidhabihu kwao kwa upendo ‘kunakubalika machoni pa Mungu.’—1 Timotheo 5:4.
-