-
Ehudi Avunja Nira ya MkandamizajiMnara wa Mlinzi—2004 | Machi 15
-
-
Simulizi hilo lililoongozwa na roho linaendelea: “Ehudi akamjia [Egloni] alipokuwa ameketi katika chumba chake cha darini chenye baridi ambacho kilikuwa chake binafsi. Naye Ehudi akaendelea kusema: ‘Nina neno linalotoka kwa Mungu kwa ajili yako.’” Ehudi hakuwa akirejelea ujumbe wa mdomo kutoka kwa Mungu. Alikuwa akifikiria tu kutumia upanga wake. Labda kwa kutarajia kusikia ujumbe fulani kutoka kwa mungu wake Kemoshi, mfalme huyo “akasimama kutoka katika kiti chake cha ufalme.”
-