Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Ajifanyia Jina Maridadi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao.

  • Yehova Ajifanyia Jina Maridadi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 63:7-

  • Yehova Ajifanyia Jina Maridadi
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 16. (a) Yehova alikuwa na maoni gani alipofanya agano lake na Israeli? (b) Mungu anashughulikaje na watu wake?

      16 Baada ya lile tukio la Kutoka, Yehova aliwaleta Israeli kwenye Mlima Sinai, akawapa ahadi hii: “Ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu . . . nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.” (Kutoka 19:5, 6) Je, Yehova alikuwa mdanganyifu kwa kuahidi hivyo? Sivyo, kwa maana Isaya anafunua kwamba Yehova alijiambia hivi yeye mwenyewe: “Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila.” Msomi mmoja anatoa maoni haya: “Neno hili ‘hakika’ halitumiwi kimamlaka ili kujionyesha kuwa na enzi kuu ya kujitawala wala kuonyesha uwezo wa kujua mambo kimbele: bali limetumiwa kuonyesha tumaini na uhakika wenye upendo.” Ndiyo, Yehova alifanya agano lake kwa nia safi, akiwa na tamaa ya moyo mweupe ya kuwasaidia watu wake wafanikiwe. Ingawa walikuwa na mapungufu ya wazi, yeye alionyesha kwamba anawaamini. Ni vizuri kama nini kuabudu Mungu anayewaamini waabudu wake! Leo, wazee wanapoonyesha kuwa hata wao wanaamini kwamba kwa msingi watu wa Mungu ni wema, hiyo husaidia sana kuwaimarisha wale waliowekwa chini ya uangalizi wao.—2 Wathesalonike 3:4; Waebrania 6:9, 10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki