Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Msiogope Ashuru
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Mstari wa 22 katika sura ya 10 waonya juu ya kuja kwa “kuangamiza” ambako kumekusudiwa. Kuangamiza huko kutakuwa kwa haki kwa sababu ni adhabu inayofaa kwa watu waasi. Tokeo ni kwamba, kutoka kwa taifa lenye wakazi wengi “kama mchanga wa pwani,” ni mabaki wachache tu watakaorudi.

  • Msiogope Ashuru
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Mstari wa 22 katika sura ya 10 waonya juu ya kuja kwa “kuangamiza” ambako kumekusudiwa. Kuangamiza huko kutakuwa kwa haki kwa sababu ni adhabu inayofaa kwa watu waasi. Tokeo ni kwamba, kutoka kwa taifa lenye wakazi wengi “kama mchanga wa pwani,” ni mabaki wachache tu watakaorudi. Mstari wa 23 waonya kuwa angamizo hilo linalokuja litaathiri nchi nzima. Yerusalemu halitaachwa salama mara hii.

      Mistari hiyo yafafanua ipasavyo mambo yaliyotukia mwaka wa 607 K.W.K. Yehova alipotumia Milki ya Babiloni kama “fimbo” yake. Nchi yote, kutia ndani Yerusalemu, ilianguka mkononi mwa mvamizi. Wayahudi walipelekwa mateka huko Babiloni kwa miaka 70. Hata hivyo, baada ya hapo baadhi yao—hata kama ni “mabaki” tu—walirudi kuanzisha upya ibada ya kweli Yerusalemu.

  • Msiogope Ashuru
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Unabii katika Isaya 10:20-23 ulikuwa na utimizo mwingine zaidi katika karne ya kwanza, kama ionyeshwavyo katika Waroma 9:27, 28. (Linganisha Isaya 1:9; Waroma 9:29.) Paulo aeleza kwamba kwa njia ya kiroho, “mabaki” ya Wayahudi ‘walimrudia’ Yehova katika karne ya kwanza W.K., kwa vile ni Wayahudi waaminifu wachache waliokuja kuwa wafuasi wa Yesu Kristo na kuanza kumwabudu Yehova “kwa roho na kweli.” (Yohana 4:24)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki