-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
6. Yatabiriwa kwamba Mesiya atakuwa mtawala wa aina gani?
6 Mesiya atakuwa mtawala wa aina gani? Je, atakuwa kama Mwashuri mkatili, mshupavu, anayeharibu ufalme wa kaskazini wa Israeli wenye makabila kumi? Sivyo hata kidogo. Isaya asema hivi kumhusu Mesiya: “Roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;
-
-
Wokovu na Kushangilia Chini ya Utawala wa MesiyaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Mesiya ateuliwa na roho takatifu ya Mungu, wala si kwa kutiwa mafuta. Jambo hilo latukia kwenye ubatizo wa Yesu, Yohana Mbatizaji aonapo roho takatifu ya Mungu iliyo kama njiwa ikiteremka juu ya Yesu. (Luka 3:22) Roho ya Yehova ‘yakaa juu ya’ Yesu, naye atoa uthibitisho wa jambo hilo atendapo kwa hekima, ufahamu, shauri, uweza, na ujuzi. Ni sifa bora kama nini anazostahili mtawala kuwa nazo!
7. Yesu aliwaahidi nini wafuasi wake waaminifu?
7 Wafuasi wa Yesu pia waweza kupokea roho takatifu. Katika mojawapo ya hotuba zake, Yesu alitangaza: “Ikiwa nyinyi, mjapokuwa waovu, mwajua jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi zilizo njema, je, si zaidi sana yule Baba aliye mbinguni atawapa roho takatifu wale wanaomwomba!” (Luka 11:13) Basi, hatupaswi kamwe kusita kumwomba Mungu roho takatifu, wala tusikome kukuza matunda yake mema—“upendo, shangwe, amani, ustahimilivu, fadhili, wema, imani, upole, kujidhibiti.” (Wagalatia 5:22, 23) Yehova aahidi kujibu maombi ya wafuasi wa Yesu yanayohusu “hekima ya kutoka juu” ili iwasaidie kukabiliana kwa mafanikio na magumu ya maisha.—Yakobo 1:5; 3:17.
8. Yesu apataje furaha katika kumcha Yehova?
8 Mesiya anamchaje Yehova? Kwa hakika, Yesu hatishwi na Mungu, akihofu hukumu yake. Badala yake, Mesiya anamcha Mungu kwa staha, staha yenye upendo kwake. Mtu mwenye kumhofu Mungu hutamani ‘kufanya sikuzote mambo yale yanayompendeza,’ kama afanyavyo Yesu. (Yohana 8:29)
-