-
Isaya Atabiri ‘Tendo la Ajabu’ la YehovaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
7. Viongozi wa Yuda wamelewaje, na matokeo ni nini?
7 Akielekeza ujumbe wake kwa Yuda, Isaya aendelea: “Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai, wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu.
-
-
Isaya Atabiri ‘Tendo la Ajabu’ la YehovaUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Yachukiza kama nini! Ulevi halisi nyumbani mwa Mungu ni mbaya sana. Lakini makuhani na manabii hao wamelewa kiroho—akili zao zimepumbazwa kwa kuitumaini mno miungano ya kibinadamu. Wamejidanganya kwa kufikiri kwamba mwendo wao ndio mwendo pekee unaofaa, labda wakiamini kwamba sasa wana mpango mwingine iwapo ulinzi wa Yehova wakosa kutosha.
-