-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
17, 18. (a) Kwa nini wahamishwa Wayahudi waweza kuitumaini ahadi ya kurudishwa? (b) Isaya auliza maswali gani yenye kutia hofu?
17 Wahamishwa Wayahudi waweza kuitumaini ahadi ya kurudishwa kwa sababu Mungu ni mwenye nguvu zote na mwenye hekima yote. Isaya asema: “Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani?
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
18 Hayo ni maswali yanayotia hofu ambayo wahamishwa Wayahudi wapaswa kuyatafakari. Je, wanadamu duni waweza kuyazuia mawimbi yenye nguvu ya bahari? Haiwezekani hata kidogo! Na bado, kwa maoni ya Yehova, bahari zinazoifunika dunia ni kama tone la maji katika kiganja cha mkono wake.b Je, wanadamu duni waweza kuzipima mbingu kubwa mno, zenye kujaa nyota au kupima milima na vilima vya dunia? La. Ingawa hivyo, Yehova huzipima mbingu kwa urahisi kama vile mwanadamu awezavyo kupima kitu fulani kwa shubiri, yaani, urefu wa kutoka mwisho wa kidole gumba hadi ncha ya kidole cha mwisho wakati mkono umenyoshwa. Ni kana kwamba Mungu aweza kuipima milima na vilima kwa mizani.
-
-
‘Wafarijini Watu Wangu’Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
b Imekadiriwa kwamba “uzito wa bahari kuu ni takriban tani kwintilioni 1.35 (1.35 x 1018), au karibu sehemu 1/4400 ya jumla ya uzito wa Dunia.”—Encarta 97 Encyclopedia.
-