Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Msiwatumainie Wakuu”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 4, 5. Yehova anawaonyeshaje watu wake upendo, lakini Yuda anaitikiaje?

      4 Swali la Yehova linalofuata linaonyesha wazi kwamba anawapenda watu wake: “Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu?” (Isaya 50:2a) Ni kana kwamba Yehova ameingia nyumbani mwa watu wake kwa kutumia watumishi wake manabii kuwasihi wamrudie kwa mioyo yao yote. Lakini wao wamekaa kimya. Wayahudi hao wanaona ni afadhali wapate msaada kwa kumtegemea mwanadamu wa ardhini, na nyakati nyingine hata wanageukia Misri.—Isaya 30:2; 31:1-3; Yeremia 37:5-7.

      5 Je, Misri ni mwokozi wa kutegemeka kuliko Yehova? Inaonekana kwamba Wayahudi hao wasio waaminifu wameyasahau matukio yaliyoongoza kwenye kuzaliwa kwa taifa lao karne nyingi mapema. Yehova anawauliza hivi: “Je! mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? au je! mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.

  • “Msiwatumainie Wakuu”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya 50:2b,

  • “Msiwatumainie Wakuu”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 6, 7. Yehova alionyeshaje nguvu zake za kuokoa wakati Misri ilipotokeza tisho?

      6 Mwaka wa 1513 K.W.K., Misri ilikuwa mkandamizi—si mkombozi aliyetumainiwa—wa watu wa Mungu. Waisraeli walikuwa watumwa katika nchi hiyo ya kipagani. Lakini Yehova akawakomboa, nao ulikuwa ukombozi wa kusisimua kama nini! Kwanza alileta Mapigo Kumi juu ya nchi hiyo. Baada ya pigo la kumi lenye maangamizi makubwa zaidi, Farao wa Misri aliwahimiza Waisraeli waondoke nchini. (Kutoka 7:14–12:31) Lakini, punde tu baada ya hapo, Farao akabadili nia. Akavikusanya vikosi vyake, akashika njia kwenda kuwashurutisha Waisraeli warudi Misri. (Kutoka 14:5-9) Jeshi la askari Wamisri likiwa nyuma ya Waisraeli, na Bahari Nyekundu ikiwa mbele yao, Waisraeli wakawa mtegoni! Lakini Yehova alikuwapo kuwapigania.

  • “Msiwatumainie Wakuu”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Hapo basi, huku majeshi ya Misri yakiwa yamebanwa, Yehova “akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu.” (Kutoka 14:21) Maji yakiisha kutenganishwa, watu wote—wanaume, wanawake, na watoto—wakaweza kuivuka salama Bahari Nyekundu. Watu wa Yehova walipofika mbali kuikaribia ng’ambo ya pili ya ufuo, Yehova akaliinua wingu. Wamisri wakatifua vumbi wakiwafuata na kujivurumisha baharini. Watu wa Yehova waliposalimika ufuoni, Yehova akayafungulia maji, yakazamisha Farao na majeshi yake. Hivyo ndivyo Yehova alivyowapigania watu wake. Lo, ni kitia-moyo kilichoje kwa Wakristo leo!—Kutoka 14:23-28.

      8. Mwishowe wakaaji wa Yuda wanaenda uhamishoni kwa kupuuza maonyo gani?

      8 Kufikia wakati wa Isaya, miaka mia saba imepita tangu kuwe na ushindi huo wa kimungu. Yuda sasa ni taifa kamili. Nyakati nyingine, linafanya mapatano ya kibalozi na serikali za kigeni, kama vile Ashuru na Misri. Lakini viongozi wa mataifa hayo ya kipagani hawatumainiki. Kila wakati, wao huweka masilahi yao wenyewe mbele ya maagano yoyote wanayoyafanya pamoja na Yuda. Manabii wanaongea kwa jina la Yehova na kuwaonya watu wasiwatumainie wanadamu hao, lakini wapi, wanaziba masikio. Mwishowe, Wayahudi watahamishiwa Babiloni wakae huko miaka 70 ya kutumikishwa. (Yeremia 25:11) Hata hivyo, Yehova hatawasahau watu wake, wala hatawatupilia mbali kwa wakati usio dhahiri. Wakati uliowekwa ukifika, atawakumbuka, awafungulie njia ya kurejea kwenye nchi yao wakarudishe ibada safi. Kwa kusudi gani? Ili wajitayarishe kwa ajili ya kuja kwa Shilo, yule atakayetiiwa na watu wote!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki