-
Kumpenda Mungu Humaanisha Nini?Mnara wa Mlinzi—1996 | Juni 15
-
-
Walipata kujua kwamba wazazi wao walikuwa wameumbwa wakiwa wakamilifu na kwamba kusudi la Yehova la awali lilikuwa kwamba wanadamu waishi milele. Huenda ikawa Adamu na Hawa waliwafafanulia lile shamba zuri la Edeni, na kwa njia fulani walihitaji kueleza ni sababu gani walikuwa wamefukuzwa kutoka makao hayo ya kiparadiso. Huenda ikawa pia Kaini na Abeli walikuwa wamejua juu ya unabii wa kimungu uliorekodiwa kwenye Mwanzo 3:15. Kupitia unabii huo Yehova alijulisha kusudi lake la kurekebisha mambo kwa wakati ufaao kwa faida ya wale wampendao na wathibitikao kuwa waaminifu-washikamanifu kwake.
Kujifunza juu ya Yehova na sifa zake lazima kuwe kulichochea katika Kaini na Abeli tamaa ya kupata kibali cha Mungu. Hivyo walimfikia Yehova kwa kumtolea matoleo. Simulizi la Biblia husema: “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili [“Abeli,” NW] naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama.”—Mwanzo 4:3, 4.
-
-
Kumpenda Mungu Humaanisha Nini?Mnara wa Mlinzi—1996 | Juni 15
-
-
Kwa nini Yehova aliikataa dhabihu ya Kaini? Je, ubora wa toleo lake ulikuwa na ubaya wowote? Je, Yehova alikuwa amekasirika kwa sababu Kaini alitoa “mazao ya ardhi” badala ya dhabihu ya mnyama? Huenda hilo lisiwe sababu. Baadaye, Mungu alikubali kwa furaha matoleo ya nafaka na mazao mengine ya ardhi kutoka kwa wengi wa waabudu wake. (Mambo ya Walawi 2:1-16) Basi, ni wazi kwamba moyo wa Kaini ulikuwa na kasoro fulani. Yehova aliweza kuusoma moyo wa Kaini naye akamwonya: “Kwa nini una ghadhabu? na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe.”—Mwanzo 4:6, 7.
-