-
DamuUfahamu wa Kina wa Maandiko
-
-
Biblia inasema kwamba uhai umo katika damu kwa sababu inahusika sana katika kuendeleza uhai. Neno la Mungu linasema hivi: “Kwa maana uhai wa kiumbe umo katika damu, nami nimeitoa kwenye madhabahu ili mwitumie kufunika dhambi zenu, kwa maana damu ndiyo inayofunika dhambi kupitia uhai ulio ndani yake.” (Law 17:11) Vilevile, Biblia inaonyesha moja kwa moja uhusiano huo inaposema: “Kwa maana uhai wa kila kiumbe ni damu yake.” (Law 17:14) Ni wazi kwamba Neno la Mungu linasema uhai na damu ni vitu vitakatifu.
-
-
DamuUfahamu wa Kina wa Maandiko
-
-
Kitabu Cyclopædia cha M’Clintock na Strong (1882, Buku la I, uku. 834) kinasema hivi kuhusu andiko la Walawi 17:11, 12: “Sheria hiyo kali haikuwahusu Waisraeli tu, bali pia wakaaji wageni walioishi miongoni mwao. Mtu aliyefanya kosa hilo ‘angeangamizwa kutoka miongoni mwa watu,’ angepata adhabu ya kifo (linganisha na Ebr. 10, 28), ingawa ni vigumu kujua kwa hakika ikiwa mtu aliuawa kwa upanga au kwa kupigwa mawe.”
-