-
Eliya Amkweza Mungu wa KweliMnara wa Mlinzi—1998 | Januari 1
-
-
Manabii wa Baali walianza ‘kuruka-ruka juu ya madhabahu waliyoifanya.’ Wakapaaza kilio tangu asubuhi wakisema: “Ee Baali, utusikie.” Lakini Baali hakujibu. (1 Wafalme 18:26) Kisha Eliya akaanza kuwadhihaki vikali akiwaambia hivi: “Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo.” (1 Wafalme 18:27) Manabii wa Baali hata walianza kujikatakata na visu na vyembe—zoea lililotumiwa mara nyingi na wapagani kuamsha sikitiko la miungu yao.b—1 Wafalme 18:28.
-
-
Eliya Amkweza Mungu wa KweliMnara wa Mlinzi—1998 | Januari 1
-
-
b Watu fulani hudokeza kwamba kujikatakata kulihusianishwa na lile zoea la kutoa dhabihu ya kibinadamu. Matendo hayo mawili yalidokeza kwamba kujitaabisha kimwili au kumwaga damu kwaweza kutokeza upendeleo wa mungu fulani.
-