-
Ziara Iliyothawabishwa SanaMnara wa Mlinzi—1999 | Julai 1
-
-
Malkia wa Sheba alivutiwa sana na hekima ya Solomoni na ufanisi wa ufalme wake hivi kwamba “roho yake ilizimia.” (1 Wafalme 10:4, 5) Wengine husema kuwa fungu hilo lamaanisha malkia “alihemahema.” Msomi mmoja hata adokeza kwamba alizimia! Hata iweje, malkia alishangazwa na yale aliyoona na kusikia. Aliwatangaza watumishi wa Solomoni kuwa wenye furaha kwa kusikiliza hekima ya mfalme huyo, naye akamtukuza Yehova kwa kumweka Solomoni kwenye kiti cha ufalme. Kisha akampa mfalme zawadi zenye thamani kubwa, dhahabu pekee ilifikia, kwa bei ya sasa, dola 40,000,000 hivi. Naye Solomoni akamtunukia zawadi, akampa malkia “haja yake yote, kila alilotaka.”c—1 Wafalme 10:6-13.
-
-
Ziara Iliyothawabishwa SanaMnara wa Mlinzi—1999 | Julai 1
-
-
c Watu fulani husema kwamba fungu hilo lamaanisha kuwa malkia alifanya ngono na Solomoni. Ngano zasema kwamba hata walipata mwana. Hata hivyo, hakuna uthibitisho unaounga mkono lolote la madai hayo.
-