Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Utawala wa “Mwana-Mfalme wa Amani” Katikati ya Maadui
    Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani”
    • 4-6. (a) Vilevile, Zaburi 2 inaonyeshaje kwamba Yesu hangengojea ulimwengu ugeuzwe kabla ya kuanza kutawala akiwa “Mwana-Mfalme wa Amani”? (b) Zaburi 2:7 ilitimizwa wakati gani?

      4 Ni wazi, basi, Yesu Kristo akiwa yule Mwana wa Daudi, hangeanza kutawala baada ya ulimwengu kugeuzwa. Badala yake, angeanza kutawala katikati ya maadui ambao kwa njia ya vita mwishowe Yehova Mungu angewaweka wawe kiti cha kuwekea miguu ya Mwanaye aliyetawazwa. Vivyo hivyo Zaburi ya pili, katika maneno yafuatayo, inaonyesha kuanza kwa utawala wake akiwa ndiye “Mwana-Mfalme wa Amani” katikati ya maadui:

      5 “Mbona mataifa wanafanya ghasia, na makabila wanatafakari ubatili? Wafalme wa dunia wanajipanga, na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya [Yehova], na juu ya masihi [Kristo wake], na tuvipasue vifungo vyao, na kuzitupia mbali nasi kamba zao. Yeye aketiye mbinguni anacheka, [Yehova] anawafanyia dhihaka. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake. Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

  • Utawala wa “Mwana-Mfalme wa Amani” Katikati ya Maadui
    Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani”
    • 7. Ni rejezo gani kwenye Zaburi 2 lililofanywa na mitume baada ya siku ya Pentekoste?

      7 Kulingana na Matendo 4:24-27, (NW) wale mitume wa Yesu Kristo, walirejeza kwenye Zaburi hii ya pili baada ya siku ya Pentekoste, 33 W.K.: “Wao kwa umoja wakainua sauti zao kwa Mungu, wakasema: ‘Bwana Mwenye Enzi Kuu, wewe Ndiwe uliyefanya mbingu na dunia na bahari na vitu vyote vilivyomo, na ambaye kupitia kwa roho takatifu ulisema kupitia kinywa cha Daudi babu yetu, mtumishi wako, “Kwa sababu gani mataifa wakawa wenye msukosuko na vikundi vya watu vikatafakari juu ya mambo yaliyo tupu? Wafalme wa dunia walichukua msimamo wao na watawala wakakusanyika pamoja kama mtu mmoja dhidi ya Yehova na dhidi ya mpakwa mafuta wake.” Ndivyo, wote wawili Herode na Pontio Pilato pamoja na watu wa mataifa pamoja na vikundi vya watu wa Israeli kwa hakika walikusanyika pamoja katika mji huu dhidi ya mtumishi mtakatifu wako Yesu, ambaye wewe ulipaka mafuta.’”

      Utimizo Mkubwa wa Zaburi 2

      8. (a) Ni wakati gani Zaburi 2:1, 2 ilipotimizwa mara ya kwanza? (b) Utimizo mkubwa wa Zaburi 2 umekuwa ukitukia tangu lini?

      8 Mwaka wa 33 wa karne ya kwanza uliona utimizo wa kwanza wa maneno hayo ya kiunabii ya Zaburi 2:1, 2. Hiyo ilikuwa ni kuhusiana na yule mwanadamu Yesu Kristo hapa duniani. Yeye alikuwa amepakwa mafuta kwa roho takatifu ya Yehova wakati alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Lakini ule utimizo mkubwa zaidi wa Zaburi 2 umekuwa ukitukia tangu mwisho wa yale Majira ya Mataifa mwaka wa 1914. (Luka 21:24, NW) Imekwisha kuthibitishwa vya kutosha kwamba zile “nyakati zilizowekwa za mataifa,” ambazo zilianza wakati wa kuharibiwa kwa mara ya kwanza kwa mji wa Yerusalemu 607 K.W.K., zilikwisha mwaka wa 1914.a Wakati huo onyo juu ya kifo lilianza kutolewa kwa mataifa ya ulimwengu huu, kutia yale ya Jumuiya ya Wakristo.

      9. Ni jambo gani lililotukia wakati wa kuharibiwa Yerusalemu kwa mara ya kwanza kuhusiana na Ufalme wa Mungu kama ulivyowakilishwa na ukoo wa kifalme wa Mfalme Daudi?

      9 Wakati wa kuharibiwa kwa Yerusalemu, na Wababuloni, ule Ufalme wa Yehova Mungu juu ya taifa la Israeli, kama ulivyowakilishwa na ukoo wa kifalme wa Mfalme Daudi ulikoma. Tangu hapo, Wayahudi wa asili hawajawa na mfalme akitawala juu yao katika ukoo wa kifalme wa nyumba ya Daudi. Lakini ule Ufalme wa Mungu Aliye Juu Zaidi ukiwa mikononi mwa mzao wa Daudi, ambaye Yehova alifanya agano la Ufalme wa milele katika ukoo wake, haungeendelea kukanyagwa milele duniani.

      10, 11. (a) Mungu alisema nini kupitia nabii wake Ezekieli kuhusiana na kiti cha ufalme cha Daudi? (b) Ni nani aliyekuja akiwa na “haki” ya kiti cha ufalme cha Daudi? (c) Umati wa Wayahudi ulisema nini alipojitoa mwenyewe akiwa yule mrithi halali?

      10 Yehova alimfanya nabii wake Ezekieli aelekeze maneno haya kwa mfalme wa Yerusalemu wa kale, kabla tu ya kuangamizwa mara ya kwanza: “Na wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kukuua, mkuu wa Israeli, ambaye siku yako imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho; Bwana [Yehova] asema hivi; Kiondoe kilemba, ivue taji; haya hayatakuwa tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka. Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa.”—Ezekieli 21:25-27.

      11 Yeye ambaye “ni haki yake” alikuja akiwa ndiye mtu Yesu Kristo, na mstari wake wa ukoo kutokana na Daudi umeandikwa kwenye Mathayo 1:1-16 na Luka 3:23-31. Yeye alitajwa na watu wengi kama “Mwana wa Daudi.” Katika ile siku alipokwenda Yerusalemu kwa shangwe, akiwa amempanda punda katika kutimiza unabii, ule umati wa Wayahudi wenye kushangilia ulioandamana naye na mitume wake ulipaza sauti kwa furaha hivi: “Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la [Yehova]; Hosana juu mbinguni.”—Mathayo 21:9

      “Mwana wa Daudi” Atawazwa Mbinguni

      12. Yesu Kristo, akiwa mrithi wa kudumu wa Daudi, alitawazwa wapi, Majira ya Mataifa yalipokwisha?

      12 Miaka 2,520 ya Mataifa kukanyaga chini ya miguu yao Ufalme wa Mungu ukiwa mikononi mwa nyumba ya Daudi ilimalizika 1914. Ndipo ulipofika wakati wa Yesu Kristo, “Mwana wa Daudi,” kutawazwa, si hapa chini kwenye kiti cha ufalme cha kidunia, bali ni katika mbingu zilizo juu zaidi kwenye mkono wa kuume wa Yehova Mungu!—Danieli 7:9, 10, 13, 14.

      13. (a) Ni tangu tarehe gani ilipoelekezwa mbele kwamba Majira ya Mataifa yangekwisha mwaka wa 1914, na ni nani walioelekeza hivyo? (b) Ni nini uliokuwa mwelekeo wa mataifa ya dunia kuhusu “Mwana wa Daudi” aliyekuwa ametawazwa?

      13 Wale waliokuja kushirikiana na Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi walikuwa wameelekeza mbele kwenye tarehe hiyo yenye maana kubwa tangu 1876. Lakini mataifa ya dunia, hata yale ya Jumuiya ya Wakristo, yalikataa kutambua kwamba huo ndio uliokuwa wakati wao wa kutoa enzi zao za kidunia kwa yule “Mwana wa Daudi” aliyekuwa ametawazwa karibuni. Wao walikataa kukubali kwamba yeye alikuwa na haki aliyopewa na Mungu ya kuwa na enzi kuu juu ya dunia yote, ambayo ni kiti cha kuwekea miguu cha Yehova Mungu. (Mathayo 5:35) Walionyesha wazi kumkataa huyo aliyekuwa na haki ya kuwa Mfalme kwa kupigana katika vita ya ulimwengu ya kwanza.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki