Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Hutujulisha Jinsi ya Kuzihesabu Siku Zetu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Novemba 15
    • 17. Kwa kawaida, watu hutarajia kuishi muda mrefu kadiri gani, nayo miaka yetu imejawa na nini?

      17 Mtunga-zaburi anasema hivi kuhusu muda ambao wanadamu wasio wakamilifu wanatarajiwa kuishi: “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; na kiburi chake ni taabu na ubatili, maana chapita upesi tukatokomea mara.” (Zaburi 90:10) Kwa ujumla, watu wanatarajiwa kuishi muda wa miaka 70, naye Kalebu alitaja kwamba alikuwa na nguvu zisizo za kawaida alipokuwa na umri wa miaka 85. Hata hivyo, kuna watu wengine walioishi muda mrefu zaidi, kama vile Aroni (123), Musa (120), na Yoshua (110). (Hesabu 33:39; Kumbukumbu la Torati 34:7; Yoshua 14:6, 10, 11; 24:29) Lakini kile kizazi kisicho na imani kilichotoka Misri, watu waliosajiliwa kuanzia miaka 20 kwenda juu walikufa katika muda wa miaka 40. (Hesabu 14:29-34) Leo, katika nchi nyingi, watu kwa kawaida hutarajia kuishi muda usiozidi huo ambao umetajwa na mtunga-zaburi. Miaka yetu imejawa na “taabu na ubatili.” Inapita upesi ‘na tunatokomea mara.’—Ayubu 14:1, 2.

  • Yehova Hutujulisha Jinsi ya Kuzihesabu Siku Zetu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Novemba 15
    • 19 Maneno ya mtunga-zaburi ni sala kwa Yehova kwamba awafundishe watu wake jinsi ya kutumia hekima katika kuzihesabu na kuzitumia siku zinazobaki za maisha yao kwa njia inayokubaliwa na Mungu. Mtu anayetarajia kuishi miaka 70 ana tumaini la kuishi siku 25,500 hivi. Lakini, hata tuwe na umri gani, ‘hatujui uhai wetu utakuwa nini kesho, kwa maana sisi ni ukungu unaotokea kwa muda kidogo na kisha kutoweka.’ (Yakobo 4:13-15) Kwa kuwa ‘wakati na tukio lisilotazamiwa hutupata sote,’ hatujui tutaishi kwa muda mrefu kadiri gani. Kwa hiyo, na tusali tuwe na hekima ya kukabiliana na majaribu, kuwatendea wengine ifaavyo, na kufanya yote tunayoweza katika utumishi wa Yehova sasa—leo! (Mhubiri 9:11; Yakobo 1:5-8) Yehova hutuongoza kupitia Neno lake, roho yake, na tengenezo lake. (Mathayo 24:45-47; 1 Wakorintho 2:10; 2 Timotheo 3:16, 17) Kutumia hekima hutuchochea ‘tutafute kwanza Ufalme wa Mungu’ na kuzitumia siku zetu katika njia inayomtukuza Yehova na kuufurahisha moyo wake. (Mathayo 6:25-33; Mithali 27:11) Bila shaka, kumwabudu kwa moyo wote hakutatuondolea matatizo yetu yote, lakini tuna hakika kwamba kufanya hivyo kutaleta baraka nyingi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki