Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mteule Wangu, Ambaye Nafsi Yangu Imependezwa Naye”!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 3. Yehova anamtumia Isaya kutoa unabii gani juu ya “mtumishi wangu”?

      3 Yehova anamtumia Isaya kutoa unabii wa kuja kwa mtumishi atakayemchagua mwenyewe: “Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu [“haki,” “NW”]. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.”—Isaya 42:1-4.

  • “Mteule Wangu, Ambaye Nafsi Yangu Imependezwa Naye”!
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 6. Yesu alijulisha haki ya kweli kwa njia zipi?

      6 Lakini, Yesu alifunua maoni ya Mungu kuhusu haki. Yesu alionyesha kwa mafundisho na maisha yake kwamba haki ya kweli ina huruma na rehema. Ebu fikiria Mahubiri yake yenye sifa ya Mlimani. (Mathayo, sura ya 5-7) Hayo ni maelezo stadi kama nini kuhusu jinsi ya kufuata haki na uadilifu! Tusomapo masimulizi ya Gospeli, je, hatuguswi moyo na huruma ya Yesu kwa maskini na wanaoonewa? (Mathayo 20:34; Marko 1:41; 6:34; Luka 7:13) Alipeleka ujumbe wake wa faraja kwa wengi waliokuwa kama mianzi iliyopondeka, iliyoinama na kupigwa huku na huku. Walikuwa kama utambi unaotoa moshi ukitaka kuzimika, uhai wao ukikaribia kufifia kabisa. Yesu hakuvunja “mwanzi uliopondeka” wala hakuzima “utambi utokao moshi.” Bali, maneno na matendo yake ya upendo na huruma yaliinua mioyo ya wapole.—Mathayo 11:28-30.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki