-
“Msiwatumainie Wakuu”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
5 Je, Misri ni mwokozi wa kutegemeka kuliko Yehova? Inaonekana kwamba Wayahudi hao wasio waaminifu wameyasahau matukio yaliyoongoza kwenye kuzaliwa kwa taifa lao karne nyingi mapema. Yehova anawauliza hivi: “Je! mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? au je! mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu. Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao.”—Isaya 50:2b, 3.
-
-
“Msiwatumainie Wakuu”Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
7 Yehova akawazima Wamisri kwa kuweka nguzo ya wingu kati yao na Waisraeli. Upande wa Wamisri wa wingu hilo kubwa kulikuwako giza, lakini katika upande wa Waisraeli kukawa na nuru. (Kutoka 14:20) Hapo basi, huku majeshi ya Misri yakiwa yamebanwa, Yehova “akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu.” (Kutoka 14:21) Maji yakiisha kutenganishwa, watu wote—wanaume, wanawake, na watoto—wakaweza kuivuka salama Bahari Nyekundu. Watu wa Yehova walipofika mbali kuikaribia ng’ambo ya pili ya ufuo, Yehova akaliinua wingu. Wamisri wakatifua vumbi wakiwafuata na kujivurumisha baharini. Watu wa Yehova waliposalimika ufuoni, Yehova akayafungulia maji, yakazamisha Farao na majeshi yake. Hivyo ndivyo Yehova alivyowapigania watu wake. Lo, ni kitia-moyo kilichoje kwa Wakristo leo!—Kutoka 14:23-28.
-