-
Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa MunguSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
17, 18. Danieli alisaidiwaje mara ya pili, na hilo lilimwezesha kufanya nini?
17 Badala ya Danieli kuchochewa na tazamio la kupokea ujumbe wenye kusisimua kama huo, yaonekana kwamba mambo aliyosikia yalikuwa yamemwathiri sana. Simulizi lataarifu hivi: “Alipokwisha kusema nami maneno hayo, nikauelekeza uso wangu chini, nikawa bubu.” Lakini malaika huyo mjumbe alikuwa tayari kutoa msaada wenye upendo—mara ya pili. Danieli alisema hivi: “Kumbe, mmoja mfano wa wanadamu akanigusa midomo yangu; ndipo nikafumbua kinywa changu, nikanena.”b—Danieli 10:15, 16a.
18 Danieli alitiwa nguvu malaika alipoigusa midomo yake. (Linganisha Isaya 6:7.) Kwa kuwa angeweza kusema tena, Danieli aliweza kumweleza malaika mjumbe magumu aliyokuwa akiyavumilia. Danieli alisema hivi: “Ee Bwana wangu, kwa sababu ya maono haya huzuni zangu zimenipata tena; hata sikusaziwa nguvu. Maana, mtumishi wa Bwana wangu huyu atawezaje kusema na Bwana wangu huyu? kwa maana kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu, wala pumzi haikusalia ndani yangu.”—Danieli 10:16b, 17.
19. Danieli alisaidiwaje mara ya tatu, na tokeo likawa nini?
19 Danieli hakuwa akilalamika wala kutoa udhuru. Alikuwa akitaja tu mashaka yake, naye malaika huyo alikubali taarifa yake. Kwa hiyo, Danieli akasaidiwa na malaika mjumbe mara ya tatu. “Mmoja mfano wa mwanadamu akanigusa tena, akanitia nguvu,” akasema nabii huyo. Baada ya kumgusa na kumtia nguvu, mjumbe huyo alisema maneno haya yenye kuliwaza: “Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu.” Mguso huo wenye upendo na maneno hayo yenye kujenga yaonekana ndiyo mambo tu aliyohitaji Danieli. Ikawaje? Danieli akatangaza hivi: “Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu.” Sasa Danieli alikuwa tayari kwa ajili ya mgawo mwingine mgumu.—Danieli 10:18, 19.
-
-
Watiwa Nguvu na Mjumbe Kutoka Kwa MunguSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
b Ingawa huenda malaika huyohuyo aliyekuwa akiongea na Danieli akawa aligusa midomo yake na kumwamsha, maneno yanayotumiwa hapa yaweza kumaanisha pia kwamba malaika mwingine, huenda Gabrieli, ndiye aliyemgusa. Hata hivyo, Danieli alitiwa nguvu na malaika mjumbe.
-