Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova Anavyowaona
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
    • 7. Yona alimtumikia Yehova chini ya hali gani huko Israeli, na kufahamu hilo kunaathirije maoni yako kumhusu?

      7 Yona alikuwa amefanya kazi ngumu kwa uaminifu huko Israeli, eneo lisilokuwa na matokeo. Nabii Amosi aliyeishi karibu wakati mmoja na Yona, alisema kwamba siku hizo Waisraeli walipenda vitu vya kimwili na anasa.b Uovu ulikuwa umeenea sana nchini, lakini Waisraeli hawakujali hata kidogo. (Amosi 3:13-15; 4:4; 6:4-6) Hata hivyo, Yona aliendelea kwa uaminifu na mgawo wake wa kuwahubiria. Ikiwa wewe ni mhubiri wa habari njema, unajua jinsi ilivyo vigumu kuzungumza na watu ambao wameridhika na maisha na wasiojali. Hivyo basi, ingawa Yona alikuwa na udhaifu, tusisahau uaminifu wake na uvumilivu wake alipowahubiria Waisraeli wasio na imani.

  • Jitahidi Kuwaona Wengine Kama Yehova Anavyowaona
    Mnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
    • b Yeroboamu wa Pili alizidisha utajiri wa ufalme wa kaskazini kutokana na ushindi mkubwa aliopata, kurudishwa kwa maeneo yaliyokuwa yametekwa, na ushuru ambao yaelekea alikusanya.—2 Samweli 8:6; 2 Wafalme 14:23-28; 2 Mambo ya Nyakati 8:3, 4; Amosi 6:2.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki