Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ibada ya Kweli Huunganisha Watu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 15
    • Muungano wa Ulimwenguni Pote Katika Wakati Wetu!

      Unabii wenye kutokeza katika kitabu cha Biblia cha Sefania unasema kuhusu kuunganishwa pamoja kwa watu wa malezi mbalimbali. Unasema hivi: “Maana hapo ndipo [mimi Yehova Mungu] nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la BWANA, wamtumikie kwa nia moja.” (Sefania 3:9) Ni jambo lenye kupendeza kama nini kuona watu waliobadilika wakimtumikia Mungu kwa muungano!

  • Ibada ya Kweli Huunganisha Watu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 15
    • Ili kuunganisha watu wake, Yehova amewapa lugha safi. Lugha hiyo mpya yatia ndani kuelewa ifaavyo kweli ya Biblia kuhusu Mungu na makusudi yake. Kuzungumza lugha safi kwahusisha kuiamini kweli, kuwafundisha wengine, na kuishi kupatana na sheria na kanuni za Mungu. Kwataka tuepuke siasa zenye kugawanya na kung’oa kabisa kutoka mioyoni mwetu mitazamo ya ubinafsi, kama vile ubaguzi wa rangi na mambo ya kizalendo ya ulimwengu huu. (Yohana 17:14; Matendo 10:34, 35) Watu wote wenye mioyo minyofu ambao wanapenda kweli wanaweza kujifunza lugha hiyo. Fikiria wale watu watano waliotajwa katika makala iliyotangulia—ambao awali walifuata dini mbalimbali—lakini sasa wameungana katika kumwabudu Mungu mmoja tu na wa pekee, Yehova.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki